Mark 9:39 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Yesu akasema, “Msimkataze, maana hakuna mtu anayefanya mwujiza kwa jina langu, na papo hapo akaweza kusema mabaya juu yangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akasema, “Msimkataze, kwa kuwa hakuna yeyote atendaye miujiza kwa Jina langu ambaye baada ya kitambo kidogo aweza kunena lolote baya dhidi yangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yesu akasema, Msimkataze, kwa kuwa hakuna mtu atakayefanya mwujiza kwa jina langu akaweza mara kuninenea mabaya;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Yesu akawaambia, “Msimzuie, kwa sababu hakuna atendaye miujiza kwa jina langu kisha mara baada ya hilo aseme maneno mabaya juu yangu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini Yesu akasema, “Msimkataze, maana hakuna mtu anayefanya muujiza kwa jina langu, na papo hapo akaweza kusema mabaya juu yangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Yesu akasema, “Msimkataze, maana hakuna mtu anayefanya mwujiza kwa jina langu, na papo hapo akaweza kusema mabaya juu yangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akasema, “Msimkataze, hakuna ye yote atendaye miujiza kwa Jina langu ambaye baada ya kitambo kidogo aweza kunena lo lote baya dhidi yangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akasema, “Msimkataze, kwa kuwa hakuna yeyote atendaye miujiza kwa Jina langu ambaye baada ya kitambo kidogo aweza kunena lolote baya dhidi yangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yesu akasema, Msimkataze, kwa kuwa hakuna mtu atakayefanya mwujiza kwa jina langu na punde baadaye akaweza kuninena kwa uovu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Yesu akasema, “Msimkataze, maana hakuna mtu anayefanya mwujiza kwa jina langu, na papo hapo akaweza kusema mabaya juu yangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yesu akasema: Msimzuie! Kwani hakuna mwenye kufanya cha nguvu kwa ajina langua atakayeweza kipunde kidogo kunisema vibaya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yesu akasema, Msimkataze, kwa kuwa hakuna mtu atakayefanya mwujiza kwa jina langu akaweza mara kuninenea mabaya;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Yesu akajibu: “Musimukataze, kwa maana hakuna mutu anayefanya miujiza kwa jina langu, ambaye anaweza nyuma kidogo kusema vibaya juu yangu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yesu akasema, Msimkataze, kwa kuwa hakuna mtu atakaefanya mwujiza kwa jina langu akaweza wakati huo huo kuninena mabaya;