Mark 9:41 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtu yeyote atakayewapeni kikombe cha maji ya kunywa, kwa sababu nyinyi ni watu wake Kristo, hakika hatakosa kupata tuzo lake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Amin, nawaambia, yeyote awapaye ninyi kikombe cha maji kwa Jina langu kwa sababu ninyi ni mali ya Al-Masihi, hakika hataikosa thawabu yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa ye yote atakayewanywesha ninyi kikombe cha maji, kwa kuwa ninyi ni watu wa Kristo, amin, nawaambia, hatakosa thawabu yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yeyote anayewapa ninyi kikombe cha maji kwa sababu ninyi ni wake Kristo. Hakika ninawaambia ukweli kwamba, hatapoteza thawabu yake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mtu yeyote atakeyewapeni kikombe cha maji ya kunywa kwa sababu ninyi ni watu wake Kristo, hakika hatakosa kupata tuzo lake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtu yeyote atakayewapeni kikombe cha maji ya kunywa, kwa sababu nyinyi ni watu wake Kristo, hakika hatakosa kupata tuzo lake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Amin, amin nawaambia, ye yote awapaye ninyi kikombe cha maji kwa Jina langu kwa sababu ninyi ni mali ya Kristo, hakika hataikosa thawabu yake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Amin, nawaambia, yeyote awapaye ninyi kikombe cha maji kwa Jina langu kwa sababu ninyi ni mali ya Al-Masihi, hakika hataikosa thawabu yake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa yeyote atakayewanywesha ninyi kikombe cha maji, kwa kuwa ninyi ni watu wa Kristo, amin, nawaambia, hatakosa thawabu yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtu yeyote atakayewapeni kikombe cha maji ya kunywa, kwa sababu nyinyi ni watu wake Kristo, hakika hatakosa kupata tuzo lake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani atakayewanywesha ninyi kinyweo cha maji tu, kwa sababu m wa Kristo, kweli nawaambiani Mshahara wake hautampotea kamwe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa ye yote atakayewanywesha ninyi kikombe cha maji, kwa kuwa ninyi ni watu wa Kristo, amin, nawaambia, hatakosa thawabu yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na yeyote atakayewapa kikombe cha maji kwa ajili yangu, kwa sababu ninyi ni watu wa Kristo, kweli ninawaambia, mutu yule hatakosa kupewa zawadi yake.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa kuwa ye yote atakaewanywesha ninyi kikombe cha maji kwa jina langu, kwa kuwa ninyi watu wa Kristo, amin nawaambieni hatakosa thawabu yake.