Mark 9:43 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mkono wako ukikukosesha, ukate! Afadhali kuingia katika uhai bila mkono mmoja, kuliko kuwa na mikono miwili na kwenda katika moto wa Jehanamu. [
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mkono wako ukikusababisha kutenda dhambi, ukate. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa na mkono mmoja, kuliko kuwa na mikono miwili lakini ukaingia Jehanamu, mahali ambako moto hauzimiki. [
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima u kigutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehanum, kwenye moto usiozimika;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ikiwa mkono wako unakusababisha ufanye dhambi, ukate. Ni bora kwako kuingia katika uzima wa milele ukiwa na mkono mmoja kuliko kuwa na mikono miwili na kuenda Jehanamu, ambako kuna moto usiozimika.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mkono wako ukikukosesha, ukate! Afadhali kuingia kwenye uzima bila mkono mmoja, kuliko kuwa na mikono miwili na kwenda katika moto wa Jehanamu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mkono wako ukikukosesha, ukate! Afadhali kuingia katika uhai bila mkono mmoja, kuliko kuwa na mikono miwili na kwenda katika moto wa Jehanamu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama mkono wako ukikusababisha kutenda dhambi, ukate. Ni afadhali kuingia katika uzima ukiwa na mkono mmoja kuliko kuwa na mikono miwili ukaingia jehanamu mahali ambako moto hauzimiki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama mkono wako ukikusababisha kutenda dhambi, ukate. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa na mkono mmoja, kuliko kuwa na mikono miwili lakini ukaingia Jehanamu, mahali ambako moto hauzimiki. [
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima ukiwa kibutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako Jehanamu, kwenye moto usiozimika; [
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mkono wako ukikukosesha, ukate! Afadhali kuingia katika uhai bila mkono mmoja, kuliko kuwa na mikono miwili na kwenda katika moto wa Jehanamu. [
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nawe, mkono wako ukikukwaza, uukate! Kuingia penye uzima mwenye kilema kutakufaa kuliko hapo, ukiwa mwenye mikono miwili, ukajiendea kuzimuni penye moto usiozimika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima u kigutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehanum, kwenye moto usiozimika; [
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama mukono wako ukikukosesha, uukate! Ni heri kwako kuingia kwenye uzima wa kweli ukiwa na mukono mumoja, kuliko kuwa na mikono miwili na kwenda katika jehenamu ndani ya moto usiozimika. [
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni kheri kuiingia katika uzima u kilema, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehannum, kwenye moto usiozimika;

Recommended Reading