Mark 9:45 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na mguu wako ukikukosesha, ukate! Afadhali kuingia katika uhai bila mguu mmoja, kuliko kuwa na miguu yote miwili na kutupwa katika moto wa Jehanamu. [
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mguu wako ukikusababisha kutenda dhambi, ukate. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili lakini ukaingia Jehanamu. [
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, u kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jehanum; [
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na ikiwa mguu wako utakusababisha ufanye dhambi, ukate. Ni bora kwako kuingia katika uzima wa milele ukiwa mlemavu kuliko kuwa na miguu miwili na kutupwa Jehanamu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Na mguu wako ukikukosesha, ukate! Afadhali kuingia katika uzima bila mguu mmoja, kuliko kuwa na miguu yote miwili na kutupwa katika moto wa Jehanamu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na mguu wako ukikukosesha, ukate! Afadhali kuingia katika uhai bila mguu mmoja, kuliko kuwa na miguu yote miwili na kutupwa katika moto wa Jehanamu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama mguu wako ukikusababisha kutenda dhambi, ukate. Ni afadhali kuingia katika uzima ukiwa kilema kuliko kuwa na miguu miwili ukaingia jehanamu mahali ambako moto hauzimiki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama mguu wako ukikusababisha kutenda dhambi, ukate. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili lakini ukaingia Jehanamu. [
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, ukiwa kiguru, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika Jehanamu; [
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na mguu wako ukikukosesha, ukate! Afadhali kuingia katika uhai bila mguu mmoja, kuliko kuwa na miguu yote miwili na kutupwa katika moto wa Jehanamu. [
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nawe, mguu wako ukikukwaza, uukate! Kuingia penye uzima, ukiwa kiwete, kutakufaa kuliko hapo, ukiwa mwenye miguu miwili, ukatupwa shimoni mwa moto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, u kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jehanum; [
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama muguu wako ukikukosesha, uukate. Ni heri kwako kuingia kwenye uzima wa kweli ukiwa na muguu mumoja, kuliko kuwa na miguu miwili na kutupwa katika moto wa jehenamu. [
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na mguu wako ukikukosesha, ukate: ni kheri kuingia katika uzima, umepungukiwa mguu, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jebannum, katika moto usiozimika;