Mark 9:47 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na jicho lako likikukosesha, lingoe! Afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu ukiwa na jicho moja tu, kuliko kuwa na macho yako yote mawili na kutupwa katika moto wa Jehanamu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nalo jicho lako likikusababisha kutenda dhambi, ling’oe. Ni afadhali kwako kuingia katika ufalme wa Mungu ukiwa na jicho moja, kuliko kuwa na macho mawili lakini ukatupwa Jehanamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na jicho lako likikukosesha, ling'oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na kama jicho lako litakusababisha ufanye dhambi, liondoe. Ni bora uingie katika Ufalme wa Mungu ukiwa na jicho moja kuliko kuwa nayo macho mawili na kutupwa Jehanamu,
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Na jicho lako likikukosesha, ling'oe! Afadhali kuingia katika utawala wa Mungu ukiwa na jicho moja tu, kuliko kuwa na macho yako yote mawili na kutupwa katika moto wa Jehanamu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na jicho lako likikukosesha, ling'oe! Afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu ukiwa na jicho moja tu, kuliko kuwa na macho yako yote mawili na kutupwa katika moto wa Jehanamu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nalo jicho lako likikusababisha kutenda dhambi, ling'oe. Ni afadhali kuwa chongo ukaingia katika Ufalme wa Mungu kuliko kuwa na macho mawili na ukatupwa jehanamu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nalo jicho lako likikusababisha kutenda dhambi, ling’oe. Ni afadhali kwako kuingia katika Ufalme wa Mwenyezi Mungu ukiwa na jicho moja, kuliko kuwa na macho mawili lakini ukatupwa Jehanamu,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na jicho lako likikukosesha, ling'oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika Jehanamu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na jicho lako likikukosesha, lingoe! Afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu ukiwa na jicho moja tu, kuliko kuwa na macho yako yote mawili na kutupwa katika moto wa Jehanamu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nalo jicho lako likikukwaza, basi, ling'oe, ulitupe mbali! Kuuingia ufalme wa Mungu mwenye chongo kutakufaa kuliko hapo, ukiwa mwenye macho mawili ukatupwa shimoni mwa moto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama jicho lako likikukosesha, uliongoe. Ni heri kwako kuingia katika Ufalme wa Mungu ukiwa na jicho moja, kuliko kuwa na macho mawili na kutupwa katika jehenamu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na jicho lako likikukosesha, litupe: ni kheri kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehannum ya moto:

Recommended Reading