Matthew 10:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu aliwaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa uwezo wa kuwafukuza pepo wachafu na kuponya magonjwa na maradhi yote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Isa akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, naye akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu, ili waweze kuwatoa na kuponya kila ugonjwa na maradhi ya kila aina.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu aliwaita pamoja wafuasi wake kumi na mbili. Akawapa uwezo juu ya pepo wabaya ili waweze kuwafukuza na pia kuponya kila aina ya magonjwa na maradhi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu aliwaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa uwezo wa kutoa pepo wachafu na kuponya magonjwa na maradhi yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu aliwaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa uwezo wa kuwafukuza pepo wachafu na kuponya magonjwa na maradhi yote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Yesu akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu kuwatoa na kuponya kila ugonjwa na maradhi ya kila aina.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Isa akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, naye akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu, ili waweze kuwatoa na kuponya kila ugonjwa na maradhi ya kila aina.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu aliwaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa uwezo wa kuwafukuza pepo wachafu na kuponya magonjwa na maradhi yote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa nguvu za kufukuza pepo wachafu na za kuponya wagonjwa wo wote na wanyonge wo wote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akawaita wanafunzi wake kumi na wawili na akawapa mamlaka ya kufukuza pepo na kuponyesha magonjwa yote na uzaifu wa kila namna.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
AKAWAITA wanafunzi wake thenashara, akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu, wawafukuze, na kuponya magonjwa yote na dhaifu zote.