Matthew 10:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama wenyeji wa nyumba hiyo wanastahili salamu hiyo, basi, amani yenu itakaa pamoja nao. Lakini ikiwa hawastahili, basi amani yenu itawarudia nyinyi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama nyumba hiyo inastahili, amani yenu na iwe juu yake. La sivyo, amani yenu na iwarudie ninyi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na nyumba ile ikistahili, amani yenu na iifikilie; la, kwamba haistahili, amani yenu na iwarudie ninyi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ikiwa watu katika nyumba hiyo watawakaribisha, wanastahili amani yenu. Wapate amani mliyowatakia. Lakini ikiwa hawatawakaribisha, hawastahili amani yenu. Ichukueni amani mliyowatakia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kama wenyeji wa nyumba hiyo wakiipokea salamu hiyo, basi, amani yenu itakaa pamoja nao. Lakini ikiwa hawaipokei, basi amani yenu itawarudia ninyi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama wenyeji wa nyumba hiyo wanastahili salamu hiyo, basi, amani yenu itakaa pamoja nao. Lakini ikiwa hawastahili, basi amani yenu itawarudia nyinyi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama nyumba hiyo inastahili, amani yenu na iwe juu yake, la sivyo, amani yenu na iwarudie ninyi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama nyumba hiyo inastahili, amani yenu na iwe juu yake. La sivyo, amani yenu na iwarudie ninyi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na nyumba ile ikistahili, amani yenu na iifikie; la, kwamba haistahili, amani yenu na iwarudie ninyi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama wenyeji wa nyumba hiyo wanastahili salamu hiyo, basi, amani yenu itakaa pamoja nao. Lakini ikiwa hawastahili, basi amani yenu itawarudia nyinyi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikiwa wamepaswa nao, utengemano wenu utakaa humo. Lakini ikiwa hawakupaswa nao, utengemano wenu utawarudia ninyi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na nyumba ile ikistahili, amani yenu na iifikilie; la, kwamba haistahili, amani yenu na iwarudie ninyi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama watu wa nyumba ile wakiwakaribisha, wakuwe na amani ile muliyowatakia, lakini wasipowakaribisha, amani ile iwarudilie.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na nyumba ile ikistahili, amani yenu iifikilie: la, haistahili, amani yenu iwarudieni.