Matthew 10:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Sasa, mimi nawatuma nyinyi kama kondoo kati ya mbwamwitu. Muwe na busara kama nyoka, na wapole kama njiwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Tazama ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa-mwitu. Kwa hiyo mwe werevu kama nyoka na wapole kama hua.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sikilizeni! Ninawatuma, nanyi mtakuwa kama kondoo katikati ya mbwa mwitu. Hivyo muwe na akili kama nyoka. Lakini pia muwe kama njiwa na msimdhuru yeyote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Sasa, mimi nawatuma ninyi kama kondoo kati ya mbwa mwitu. Muwe na busara kama nyoka, na wapole kama njiwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Sasa, mimi nawatuma nyinyi kama kondoo kati ya mbwamwitu. Muwe na busara kama nyoka, na wapole kama njiwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Tazama, ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu. Kwa hiyo mwe werevu kama nyoka na wapole kama hua.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Tazama, ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu. Kwa hiyo mwe werevu kama nyoka na wapole kama hua.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwamwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Sasa, mimi nawatuma nyinyi kama kondoo kati ya mbwamwitu. Muwe na busara kama nyoka, na wapole kama njiwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tazameni, mimi nawatuma, mwe kama kondoo walio katikati ya mbwa wa mwitu. Kwa hiyo mwe wenye mizungu kama nyoka, tena mwe wakweli, kama njiwa walivyo! Jilindeni kwa ajili ya watu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Muangalie! Ninawatuma kama kondoo katikati ya imbwa wa pori. Basi mukuwe waangalifu kama nyoka na wakamilifu kama njiwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Angalieni, mimi nawatumeni kama kondoo kati ya mbwa wa mwitu: bassi mwe na busara kama nyoka, na msio na dhara kama hua.