Matthew 10:17 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jihadharini na watu, maana watawapeleka nyinyi mahakamani na kuwapiga viboko katika masunagogi yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka katika mabaraza yao na kuwapiga kwenye masinagogi yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka mabarazani, na katika masinagogi yao watawapiga;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Muwe waangalifu! Wapo watu watakaowakamata na kuwapeleka ili kuwashitaki mbele ya mabaraza ya mijini. Watawachapa ndani ya masinagogi yao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Jihadharini na watu, maana watawapeleka ninyi mahakamani na kuwapiga viboko katika masunagogi yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jihadharini na watu, maana watawapeleka nyinyi mahakamani na kuwapiga viboko katika masunagogi yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Jihadharini na wanadamu, kwa maana watawapeleka katika mabaraza yao na kuwapiga kwenye masinagogi yao,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka katika mabaraza yao na kuwapiga kwenye masinagogi yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka mabarazani, na katika masinagogi yao watawapiga;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jihadharini na watu, maana watawapeleka nyinyi mahakamani na kuwapiga viboko katika masunagogi yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani watawapeleka barazani kwao wakuu na kuwapiga katika nyumba zao za kuombea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka mabarazani, na katika masinagogi yao watawapiga;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mujilinde, kwa maana watu watawapeleka mbele ya tribinali kubwa nao watawapiga fimbo ndani ya nyumba zao za kuabudia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Jihadharini na wana Adamu; kwa maana watawapelekeni mbele ya baraza, na katika masunagogi yao watawapiga;