Matthew 10:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtapelekwa mbele ya watawala na wafalme kwa sababu yangu, mpate kunishuhudia kwao na kwa watu wa mataifa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nanyi mtaburutwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, ili kuwa ushuhuda kwao na kwa watu wa Mataifa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mtasimamishwa mbele ya magavana na wafalme. Watu watawafanyia ninyi hivi kwa sababu mnanifuata. Mtakuwa mashahidi wangu mbele za wafalme na magavana hao na kwa watu wa mataifa mengine.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mtapelekwa mbele ya watawala na wafalme kwa sababu yangu, mpate kutangaza Habari Njema kwao na kwa mataifa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtapelekwa mbele ya watawala na wafalme kwa sababu yangu, mpate kunishuhudia kwao na kwa watu wa mataifa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
nanyi mtaburutwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, ili kuwa ushuhuda kwao na mbele ya watu Mataifa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nanyi mtaburutwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, ili kuwa ushuhuda kwao na kwa watu wa Mataifa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nanyi mtachukuliwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtapelekwa mbele ya watawala na wafalme kwa sababu yangu, mpate kunishuhudia kwao na kwa watu wa mataifa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa ajili yangu watawavuta kwa mabwana wakubwa na kwa wafalme, mje mnishuhudie kwao na kwa wamizimu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile mutapelekwa mbele ya wakubwa na wafalme kwa ajili yangu, kusudi mutoe ushuhuda wangu mbele yao na mbele ya watu wa mataifa mengine.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, illi kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa.