Matthew 10:25 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yatosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumishi kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mkubwa wa jamaa Beelzebuli, je, hawatawaita watu wengine wa jamaa hiyo majina mabaya zaidi?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yatosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumishi kuwa kama bwana wake. Ikiwa mkuu wa nyumba ameitwa Beelzebuli, je, si watawaita zaidi wale wa nyumbani mwake!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumwa kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebuli, je! Si zaidi wale walio wa nyumbani mwake?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Inatosha kwa wanafunzi kuwa kama walimu wao na watumwa kuwa kama bwana wao. Iwapo watu hao wananiita ‘mtawala wa pepo’, na mimi ni kiongozi wa familia, basi ni dhahiri kwa kiasi gani watawatukana ninyi, mlio familia yangu!
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yatosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumishi kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mkubwa wa jamaa Beelzebuli, je hawatawaita watu wengine wa jamaa hiyo majina mabaya zaidi?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yatosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumishi kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mkubwa wa jamaa Beelzebuli, je, hawatawaita watu wengine wa jamaa hiyo majina mabaya zaidi?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yatosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake na mtumishi kuwa kama bwana wake. Ikiwa mkuu wa nyumba ameitwa Beelzebuli, je, si zaidi sana wale wa nyumbani mwake mwenyewe!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yatosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumishi kuwa kama bwana wake. Ikiwa mkuu wa nyumba ameitwa Beelzebuli, je, si watawaita zaidi wale wa nyumbani mwake!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumwa kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebuli, je! Si zaidi wale walio wa nyumbani mwake?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yatosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumishi kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mkubwa wa jamaa Beelzebuli, je, hawatawaita watu wengine wa jamaa hiyo majina mabaya zaidi?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Inamtosha mwanafunzi kuwa, kama mfunzi wake alivyo, vilevile mtumwa inamtosha kuwa, kama bwana wake alivyo. Kama Mwenye nyumba walimwita Belzebuli (Mkuu wa pepo), hawatazidi kuwaita hivyo waliomo nyumbani mwake?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumwa kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebuli, je! Si zaidi wale walio wa nyumbani mwake?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini inatosha kwa mwanafunzi kufanana na mwalimu wake na mutumishi kufanana na bwana wake. Ikiwa wanamwita mukubwa wa jamaa Belzebuli, hawatakosa kuwaita watu wa jamaa yake kwa majina mabaya zaidi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumishi kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebul, je, si zaidi wale walio nyumbani mwake?