Matthew 10:37 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ampendaye baba au mama yake kuliko anipendavyo mimi, hanistahili. Ampendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Yeyote ampendaye baba yake au mama yake kuliko anavyonipenda mimi, hastahili kuwa wangu. Yeyote ampendaye mwanawe au binti yake kuliko anavyonipenda mimi, hastahili kuwa wangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wale wanaowapenda baba zao au mama zao kuliko wanavyonipenda mimi hawana thamani kwangu. Na wale wanaowapenda wana wao au binti zao kuliko wanavyonipenda mimi hawastahili kuwa wafuasi wangu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Ampendaye baba au mama yake kuliko anipendavyo mimi, hanistahili. Ampendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ampendaye baba au mama yake kuliko anipendavyo mimi, hanistahili. Ampendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ye yote ampendaye baba yake au mama yake kuliko anavyonipenda mimi, hastahili kuwa wangu. Ye yote ampendaye mwanawe au binti yake kuliko anavyonipenda Mimi, hastahili kuwa wangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Yeyote ampendaye baba yake au mama yake kuliko anavyonipenda mimi, hastahili kuwa wangu. Yeyote ampendaye mwanawe au binti yake kuliko anavyonipenda mimi, hastahili kuwa wangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Ampendaye baba au mama yake kuliko anipendavyo mimi, hanistahili. Ampendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Anayempenda baba yake au mama yake kuliko mimi hanipasi; anayempenda mwanawe wa kiume au wa kike kuliko mimi hanipasi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Yeye anayemupenda baba yake au mama yake kuliko mimi, hastahili kuwa wangu, na yeyote anayemupenda mwana wake au binti yake kuliko mimi hastahili kuwa wangu vilevile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Apendae baba au mama kuliko mimi, hanifai; na apendae mwana au binti kuliko mimi hanifai.