Matthew 10:5 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu aliwatuma hao kumi na wawili na kuwapa maagizo haya: “Msiende kwa watu wa mataifa mengine, wala msiingie katika miji ya Wasamaria.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hawa kumi na wawili, Isa aliwatuma akawaagiza: “Msiende miongoni mwa watu wa Mataifa, wala msiingie mji wowote wa Wasamaria.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hao Thenashara Yesu aliwatuma, akawaagiza, akisema, Katika njia ya Mataifa msiende, wala katika mji wo wote wa Wasamaria msiingie.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu aliwatuma mitume hawa kumi na wawili pamoja na maelekezo haya: “Msiende kwa watu wasio Wayahudi. Na msiingie katika miji ambako Wasamaria wanaishi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu aliwatuma hao kumi na wawili na kuwapa maagizo haya: “Msiende kwa watu wa mataifa mengine, wala msiingie katika mji wa Wasamaria.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu aliwatuma hao kumi na wawili na kuwapa maagizo haya: “Msiende kwa watu wa mataifa mengine, wala msiingie katika miji ya Wasamaria.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hawa kumi na wawili, Yesu aliwatuma akawaagiza, “Msiende miongoni mwa watu Mataifa wala msiingie mji wo wote wa Wasamaria.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hawa kumi na wawili, Isa aliwatuma akawaagiza: “Msiende miongoni mwa watu wa Mataifa, wala msiingie mji wowote wa Wasamaria.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hao Kumi na Wawili Yesu aliwatuma, akawaagiza, akisema, Katika njia ya Mataifa msiende, wala katika mji wowote wa Wasamaria msiingie.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu aliwatuma hao kumi na wawili na kuwapa maagizo haya: “Msiende kwa watu wa mataifa mengine, wala msiingie katika miji ya Wasamaria.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hao kumi na wawili Yesu aliwatuma na kuwaagiza akisema: Msiende katika njia za wamizimu, wala mji wowote wa Wasamaria msiuingie!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hao Thenashara Yesu aliwatuma, akawaagiza, akisema, Katika njia ya Mataifa msiende, wala katika mji wo wote wa Wasamaria msiingie.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hao ndio wanafunzi kumi na wawili Yesu aliowatuma, akiwaagiza mambo haya: “Musiende katika inchi za watu wa mataifa mengine wala musiingie katika muji wowote wa Samaria.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hawa thenashara Yesu aliwatuma, akawaagiza, akinena, Katika njia ya Mataifa msiende, wala mjini mwa Wasamaria msiingie: