Matthew 11:18 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa maana Yohane alikuja, akafunga na wala hakunywa divai, nao wakasema: ‘Amepagawa na pepo’.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana Yahya alikuja, alikuwa hali wala hanywi, nao wanasema, ‘Yeye ana pepo mchafu.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana Yohana alikuja, hali wala hanywi, wakasema, Yuna pepo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa nini ninasema watu wako hivyo? Kwa sababu Yohana alikuja na hakula vyakula vya kawaida na kunywa divai, na watu walisema, ‘Ana pepo ndani yake.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa maana Yohane alikuja, akafunga na wala hakunywa divai, nao wakasema: Amepagawa na pepo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa maana Yohane alikuja, akafunga na wala hakunywa divai, nao wakasema: ‘Amepagawa na pepo’.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana Yohana Mbatizaji alikuja hali wala hanywi, nao wanasema, ‘Yeye ana pepo mchafu.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana Yahya alikuja, alikuwa hali wala hanywi, nao wanasema, ‘Yeye ana pepo mchafu.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana Yohana alikuja, hali wala hanywi, wakasema, Ana pepo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa maana Yohane alikuja, akafunga na wala hakunywa divai, nao wakasema: ‘Amepagawa na pepo’.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Yohana alikuja, hakula, wala hakunywaakala, wakasema: Ana pepo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana Yohana alikuja, hali wala hanywi, wakasema, Yuna pepo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana Yoane alikuja, alifunga kula chakula na kunywa, nao wakasema: ‘Yuko na pepo!’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana Yohana alikuja, hali wala hanywi, wakanena. Yuna pepo.