Matthew 11:19 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwana wa Mtu akaja, anakula na kunywa, nao wakasema: ‘Mwangalieni huyu, mlafi na mlevi, rafiki yao watozaushuru na wenye dhambi!’ Hata hivyo, hekima ya Mungu inathibitishwa kuwa njema kutokana na matendo yake.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwana wa Adamu alikuja akila na kunywa, nao wanasema, ‘Tazameni huyu mlafi na mlevi, rafiki wa watoza ushuru na “wenye dhambi.” ’ Lakini hekima huthibitishwa kuwa kweli kwa matendo yake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakasema, Mlafi huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa kazi zake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mwana wa Adamu amekuja akila na kunywa, na watu husema, ‘Mwangalie! Hula sana na kunywa divai nyingi. Ni rafiki wa wakusanya kodi na wenye dhambi wengine.’ Lakini hekima inaonesha kuwa sahihi kutokana na yale inayotenda.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mwana wa Mtu akaja, anakula na kunywa, nao wakasema: Mtazameni huyu, mlafi na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wahalifu! Hata hivyo, hekima ya Mungu inathibitishwa kuwa njema kutokana na matendo yake.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwana wa Mtu akaja, anakula na kunywa, nao wakasema: ‘Mwangalieni huyu, mlafi na mlevi, rafiki yao watozaushuru na wenye dhambi!’ Hata hivyo, hekima ya Mungu inathibitishwa kuwa njema kutokana na matendo yake.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwana wa Adamu alikuja akila na kunywa, nao wanasema, ‘Tazama, mlafi na mlevi, rafiki wa watoza ushuru na “wenye dhambi.” ’ Lakini hekima huthibitishwa kwa haki ya matendo yake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwana wa Adamu alikuja akila na kunywa, nao wanasema, ‘Tazameni huyu mlafi na mlevi, rafiki wa watoza ushuru na “wenye dhambi.” ’ Lakini hekima huthibitishwa kuwa kweli kwa matendo yake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakasema, Mlafi huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa kazi zake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwana wa Mtu akaja, anakula na kunywa, nao wakasema: ‘Mwangalieni huyu, mlafi na mlevi, rafiki yao watozaushuru na wenye dhambi!’ Hata hivyo, hekima ya Mungu inathibitishwa kuwa njema kutokana na matendo yake.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwana wa mtu alikuja, akala, akanywa, wakasema: Tazameni mtu huyu mlaji na mnyuwaji wa mvinyo, mpenda watoza kodi na wakosaji! Lakini werevu hutokezwa na matendo yake kuwa wa kweli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakasema, Mlafi huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa kazi zake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwana wa Mutu alikuja, yeye anakula na kunywa, nao wanasema: ‘Angalia huyu mulafi na mulevi, rafiki wa walipishaji wa kodi na watenda maovu wenzao.’ Lakini hekima ya Mungu ilionyeshwa kuwa ya haki kwa njia ya matendo yake.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakanena, Mlafi huyu, na mnywa mvinyo, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imepewa haki na watoto wake.