Matthew 11:20 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Yesu akaanza kuilaumu miji ambayo, ingawaje alifanya miujiza mingi humo, watu wake hawakutaka kutubu:
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Isa akaanza kuishutumu miji ambayo alifanya miujiza yake mingi, kwa maana watu wake hawakutubu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo akaanza kuikemea miji ile ambamo ndani yake ilifanyika miujiza yake iliyo mingi, kwa sababu haikutubu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha Yesu akaanza kuikosoa miji ambako alifanya miujiza yake mingi. Aliikosoa miji hii kwa sababu watu katika miji hii hawakubadili maisha yao na kuacha kutenda dhambi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha Yesu akaanza kuilaumu miji ambayo, ingawaje alifanya miujiza mingi humo, watu wake hawakutaka kubadili nia zao mbaya:
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Yesu akaanza kuilaumu miji ambayo, ingawaje alifanya miujiza mingi humo, watu wake hawakutaka kutubu:
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Yesu akaanza kushutumu miji ambamo alifanya miujiza yake mingi kuliko kwingine, kwa maana watu wake hawakutubu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Isa akaanza kushutumu miji ambamo alifanya miujiza yake mingi kuliko kwingine, kwa maana watu wake hawakutubu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo akaanza kuikemea miji ile ambamo ndani yake ilifanyika miujiza yake iliyo mingi, kwa sababu haikutubu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Yesu akaanza kuilaumu miji ambayo, ingawaje alifanya miujiza mingi humo, watu wake hawakutaka kutubu:
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo Yesu alipoanza kuikaripia miji, yalimofanyika ya nguvu yake mengi, kwa maana haikujuta.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo akaanza kuikemea miji ile ambamo ndani yake ilifanyika miujiza yake iliyo mingi, kwa sababu haikutubu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Yesu akaanza kuonya miji ambamo alifanya miujiza mingi zaidi, kwa sababu wakaaji wa kule hawakugeuka toka zambi zao. Akasema:
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ndipo akaanza kuikemea miji ile ambamo ilifanyika miujiza yake iliyo mingi, kwa sababu haikutubu.