Matthew 11:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na wewe Kafarnaumu, je, utajikweza mpaka mbinguni? Utaporomoshwa mpaka kuzimu! Maana, kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika kule Sodoma, mji huo ungalikuwako mpaka hivi leo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nawe Kapernaumu, je, utainuliwa hadi mbinguni? La hasha! Utashushwa hadi Kuzimu. Miujiza iliyofanyika kwako ingefanyika huko Sodoma, mji huo ungekuwepo hadi leo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo hata leo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nawe Kapernaumu, utakwezwa mpaka mbinguni? Hapana! Utatupwa chini mpaka Kuzimu. Nimetenda miujiza mingi ndani yako. Iwapo miujiza hii ingetokea Sodoma, watu huko wangeacha kutenda dhambi na ungekuwa bado ni mji hata leo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Na wewe Kafarnaumu, je, utajikweza mpaka mbinguni? Utaporomoshwa mpaka Kuzimu! Maana, kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika kule Sodoma, mji huo ungalikuwako mpaka hivi leo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na wewe Kafarnaumu, je, utajikweza mpaka mbinguni? Utaporomoshwa mpaka kuzimu! Maana, kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika kule Sodoma, mji huo ungalikuwako mpaka hivi leo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nawe Kapernaumu, je, utainuliwa hadi mbinguni? La hasha, utashushwa pande za chini sana. Miujiza iliyofanyika kwako ingefanyika huko Sodoma, mji huo ungalikuwapo hadi leo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nawe Kapernaumu, je, utainuliwa hadi mbinguni? La hasha, utashushwa mpaka kuzimu. Miujiza iliyofanyika kwako ingefanyika huko Sodoma, mji huo ungalikuwepo hadi leo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo hata leo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na wewe Kafarnaumu, je, utajikweza mpaka mbinguni? Utaporomoshwa mpaka kuzimu! Maana, kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika kule Sodoma, mji huo ungalikuwako mpaka hivi leo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nawe Kapernaumu, hukupazwa mpaka mbinguni? Utatumbukia mpaka kuzimuni, kwani ya nguvu yaliyofanyika kwako, kama yangalifanyika Sodomu, ungalikuwako mpaka leo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo hata leo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nawe, muji Kapernaumu, unafikiri kwamba utapandishwa mpaka juu mbinguni? Utashushwa mpaka chini katika kuzimu. Kwa maana miujiza iliyofanyika ndani yako ingalifanyika katika Sodoma, muji ule ungekuwa ungali hata leo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nawe Kapernaum, uliyeinuliwa hatta mbinguni, utashushwa hatta kuzimu: kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwako, ingalifanyika katika Sodom, ungalikuwapo hatta leo.