Matthew 11:27 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Baba yangu amenikabidhi vitu vyote. Hakuna amjuaye Mwana ila Baba, wala amjuaye Baba ila Mwana, na yeyote yule ambaye Mwana anapenda kumfunulia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nimekabidhiwa vitu vyote na Baba yangu: Hakuna mtu amjuaye Mwana ila Baba, wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana na yeyote ambaye Mwana anapenda kumfunulia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Nimekabidhiwa vyote na baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baba yangu amenipa kila kitu. Hakuna amjuaye Mwana isipokuwa Baba peke yake. Na hakuna amjuaye Baba isipokuwa Mwana ndiye anayemjua Baba. Na watu pekee watakaomjua Baba ni wale ambao Mwana atachagua kuwaonesha.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Baba yangu amenikabidhi vitu vyote. Hakuna amjuaye Mwana ila Baba, wala amjuaye Baba ila Mwana, na yeyote yule ambaye Mwana atapenda kumjulisha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Baba yangu amenikabidhi vitu vyote. Hakuna amjuaye Mwana ila Baba, wala amjuaye Baba ila Mwana, na yeyote yule ambaye Mwana anapenda kumfunulia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Nimekabidhiwa vitu vyote na Baba yangu: Hakuna mtu amjuaye Mwana ila Baba, wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana na ye yote ambaye Mwana anapenda kumdhihirisha Baba kwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Nimekabidhiwa vitu vyote na Baba yangu: Hakuna mtu amjuaye Mwana ila Baba, wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana na yeyote ambaye Mwana anapenda kumfunulia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na yeyote ambaye Mwana apenda kumfunulia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Baba yangu amenikabidhi vitu vyote. Hakuna amjuaye Mwana ila Baba, wala amjuaye Baba ila Mwana, na yeyote yule ambaye Mwana anapenda kumfunulia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vyote nimepewa na Baba yangu. Hakuna anayemtambua Mwana pasipo Baba; wala hakuna anayemtambua Baba pasipo mwana na kila, Mwana atakayemfunulia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Nimekabidhiwa vyote na baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Baba yangu ameweka vitu vyote katika mikono yangu. Hakuna mutu anayemujua Mwana isipokuwa Baba, wala hakuna anayemujua Baba isipokuwa Mwana, na yeyote Mwana anayetaka kumujulisha kwake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu: wala hakuna mtu amjuae Mwana, illa Baba; wala hakuna mtu amjuae Baba illa Mwana, na ye yote ambae Mwana apenda kumfunulia.