Matthew 12:2 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mafarisayo walipoona hayo, wakamwambia Yesu, “Tazama, wanafunzi wako wanafanya jambo lisilo halali kufanya siku ya Sabato.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Mafarisayo walipoona jambo hili, wakamwambia, “Tazama! Wanafunzi wako wanafanya jambo lisilo halali kufanywa siku ya Sabato.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Mafarisayo walipoona, walimwambia, Tazama! Wanafunzi wako wanafanya neno ambalo si halali kulifanya siku ya sabato.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mafarisayo walioliona hili, wakamwambia Yesu, “Tazama! Wafuasi wako wanafanya kitu ambacho ni kinyume na sheria yetu kufanya katika siku ya Sabato.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mafarisayo walipoona hayo, wakamwambia Yesu, “Tazama, wanafunzi wako wanafanya jambo ambalo si halali siku ya Sabato.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mafarisayo walipoona hayo, wakamwambia Yesu, “Tazama, wanafunzi wako wanafanya jambo lisilo halali kufanya siku ya Sabato.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Mafarisayo walipoona jambo hili, wakamwambia, “Tazama! Wanafunzi wako wanafanya jambo lisilo halali siku ya Sabato.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Mafarisayo walipoona jambo hili, wakamwambia, “Tazama! Wanafunzi wako wanafanya jambo lisilo halali kufanywa siku ya Sabato.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Mafarisayo walipoona, walimwambia, Tazama! Wanafunzi wako wanafanya jambo ambalo si halali kulifanya siku ya sabato.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mafarisayo walipoona hayo, wakamwambia Yesu, “Tazama, wanafunzi wako wanafanya jambo lisilo halali kufanya siku ya Sabato.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Mafariseo walipoviona wakamwambia: Tazama, wanafunzi wako wanafanya yaliyo mwiko kuyafanya siku ya mapumziko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Mafarisayo walipoona, walimwambia, Tazama! Wanafunzi wako wanafanya neno ambalo si halali kulifanya siku ya sabato.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wafarisayo walipoona mambo hayo, wakamwambia Yesu: “Angalia! Wanafunzi wako wanafanya mambo yanayokatazwa kufanya kwa siku ya Sabato!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na Mafarisayo walipoona, wakamwambia, Tazama! wanafunzi wako wanatenda lililo haramu kutenda siku ya sabato.