Matthew 12:20 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala utambi ufukao moshi hatauzima, mpaka atakapoifanya hukumu ya haki itawale.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwanzi uliopondeka hatauvunja, na utambi unaofuka moshi hatauzima, hadi atakapoifanya haki ishinde.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwanzi uliopondeka hatauvunja, Wala utambi utokao moshi hatauzima, Hata ailetapo hukumu ikashinda.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hatavunja wala kupindisha unyasi. Hatazimisha hata mwanga hafifu. Hatashindwa mpaka ameifanya haki kuwa mshindi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala utambi ufukao moshi hatauzima, mpaka atakapoifanya hukumu ya haki itawale.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala utambi ufukao moshi hatauzima, mpaka atakapoifanya hukumu ya haki itawale.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwanzi uliopondeka hatauvunja, utambi unaofuka moshi hatauzima, mpaka atakapoifanya haki ishinde.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwanzi uliopondeka hatauvunja, na utambi unaofuka moshi hatauzima, mpaka atakapoifanya haki ishinde.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwanzi uliopondeka hatauvunja, Wala utambi utokao moshi hatauzima, Hadi ailetapo hukumu ikashinda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala utambi ufukao moshi hatauzima, mpaka atakapoifanya hukumu ya haki itawale.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Utete uliopondeka hatauvunja kabisa, wala utambi unaotoka moshi bado hatauzima, mpaka aitokeze ile hukumu kuwa ya kushinda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwanzi uliopondeka hatauvunja, Wala utambi utokao moshi hatauzima, Hata ailetapo hukumu ikashinda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hatavunja tete linalokunja, wala hatazimisha taa inayofifia, mpaka aiwezeshe haki kutawala.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mwanzi uliopondeka hatauvunja, Wala kitani kitokacho moshi hatakizima, Hatta aletapo hukumu yake ikashinda.