Matthew 12:28 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini ikiwa ninawafukuza pepo kwa nguvu ya Roho wa Mungu, basi jueni kwamba ufalme wa Mungu umekwisha fika kwenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kama mimi ninatoa pepo wachafu kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekuja juu yenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini mimi nikitoa pepo kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini ninatumia nguvu ya Roho wa Mungu kuyafukuza mashetani, na hili linaonesha kuwa Ufalme wa Mungu umekuja kwenu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini ikiwa ninawafukuza pepo kwa nguvu ya Roho wa Mungu, basi jueni kwamba Ufalme wa Mungu umekwisha fika kwenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini ikiwa ninawafukuza pepo kwa nguvu ya Roho wa Mungu, basi jueni kwamba ufalme wa Mungu umekwisha fika kwenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kama mimi ninatoa pepo wachafu kwa Roho wa Mungu, basi Ufalme wa Mungu umekuja juu yenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kama mimi ninatoa pepo wachafu kwa Roho wa Mwenyezi Mungu, basi Ufalme wa Mwenyezi Mungu umekuja juu yenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini mimi nikitoa pepo kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini ikiwa ninawafukuza pepo kwa nguvu ya Roho wa Mungu, basi jueni kwamba ufalme wa Mungu umekwisha fika kwenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mimi nikiwafukuza pepo kwa nguvu ya Roho ya Mungu, ufalme wa Mungu umekwisha kuwafikia ninyi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini mimi nikitoa pepo kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa ngambo yangu ninafukuza pepo kwa uwezo wa Roho wa Mungu. Hii inaonyesha kwamba Ufalme wa Mungu umekwisha kufika kati yenu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini mimi nikifukuza pepo kwa uweza wa Bobo ya Mungu, bassi ufalme wa Mungu umekujieni.