Matthew 12:31 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa sababu hiyo, nawaambieni, watu watasamehewa dhambi na kufuru zao zote, lakini hawatasamehewa dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo nawaambia, kila dhambi na kufuru watu watasamehewa, lakini mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu wa Mungu hatasamehewa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo ninawaambia, Mungu atawasamehe watu kila dhambi wanayotenda au kila jambo baya wanalosema kinyume naye. Lakini yeyote anayesema kinyume na Roho Mtakatifu hatasamehewa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa sababu hiyo, nawaambieni, watu watasamehewa dhambi na kufuru zao zote, lakini hawatasamehewa dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa sababu hiyo, nawaambieni, watu watasamehewa dhambi na kufuru zao zote, lakini hawatasamehewa dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo nawaambia, kila dhambi na kufuru watu watasamehewa, lakini mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo nawaambia, kila dhambi na kufuru watu watasamehewa, lakini mtu atakayemkufuru Roho wa Mwenyezi Mungu hatasamehewa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa sababu hiyo, nawaambieni, watu watasamehewa dhambi na kufuru zao zote, lakini hawatasamehewa dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo nawaambiani: Kila kosa na kila neno la kumbeza Mungu watu wataondolewa, lakini la kumbeza Roho hawataondolewa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo ninawaambia: watu wataweza kusamehewa zambi zote wanazofanya na matusi yao yote. Lakini mutu anayetukana Roho Mutakatifu hatasamehewa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa sababu hii nawaambieni, Killa dhambi na killa neno la kufuru watasamehewa wana Adamu, bali kumtukana Roho hawatasamehewa wana Adamu.