Matthew 12:33 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake yatakuwa mazuri; ufanyeni kuwa mbaya na matunda yake yatakuwa mabaya. Mti hujulikana kwa matunda yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ufanye mti kuwa mzuri, nayo matunda yake yatakuwa mazuri. Au ufanye mti kuwa mbaya, na matunda yake yatakuwa mabaya. Kwa maana mti hutambulika kwa matunda yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri; au ufanyeni mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ikiwa unataka matunda mazuri, ni lazima uutunze mti vizuri. Ikiwa mti wako siyo mzuri, utakuwa na matunda mabaya. Mti unajulikana kutokana na aina ya matunda inaozalisha.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake yatakuwa mema; ufanyeni kuwa mbaya na matunda yake yatakuwa mabaya. Mti hujulikana kwa matunda yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake yatakuwa mazuri; ufanyeni kuwa mbaya na matunda yake yatakuwa mabaya. Mti hujulikana kwa matunda yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ufanye mti kuwa mzuri nayo matunda yake yatakuwa mazuri, au ufanye mti kuwa mbaya na matunda yake yatakuwa mabaya, kwa maana mti hutambulikana kwa matunda yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ufanye mti kuwa mzuri, nayo matunda yake yatakuwa mazuri. Au ufanye mti kuwa mbaya, na matunda yake yatakuwa mabaya. Kwa maana mti hutambulika kwa matunda yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri; au ufanyeni mti kuwa mbaya na matunda yake kuwa mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake yatakuwa mazuri; ufanyeni kuwa mbaya na matunda yake yatakuwa mabaya. Mti hujulikana kwa matunda yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mkipanda mti nzuri, basi mtapata hata matunda mazuri. Au mkipanda mti mwovu, basi, mtapata hata matunda maovu. Kwani mti hutambulikana kwa matunda yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri; au ufanyeni mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Muti ukiwa muzuri, matunda yake yatakuwa mazuri vilevile; nao muti ukiwa mubaya, matunda yake yatakuwa mabaya vilevile. Kwa maana muti unatambulikana kwa matunda yake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri; au ufanyeni mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hujulikana.