Matthew 12:35 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtu mwema hutoa mambo mema katika hazina yake njema; na mtu mbaya hutoa mambo mabaya katika hazina yake mbaya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutoka hazina ya mambo mema yaliyohifadhiwa ndani yake, naye mtu mwovu hutoa yaliyo maovu kutoka hazina ya mambo maovu yaliyohifadhiwa ndani yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Walio wema wana vitu vizuri vilivyotunzwa katika mioyo yao. Ndiyo maana husema mambo mazuri. Lakini wale walio waovu wana mioyo iliyojaa uovu, na ndiyo sababu husema mambo maovu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mtu mwema hutoa mambo mema katika hazina yake njema; na mtu mbaya hutoa mambo mabaya katika hazina yake mbaya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtu mwema hutoa mambo mema katika hazina yake njema; na mtu mbaya hutoa mambo mabaya katika hazina yake mbaya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutoka katika hazina ya mambo mema yaliyohifadhiwa ndani yake, naye mtu mwovu hutoa yaliyo maovu kutoka katika hazina ya mambo maovu yaliyohifadhiwa ndani yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutoka hazina ya mambo mema yaliyohifadhiwa ndani yake, naye mtu mwovu hutoa yaliyo maovu kutoka hazina ya mambo maovu yaliyohifadhiwa ndani yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtu mwema hutoa mambo mema katika hazina yake njema; na mtu mbaya hutoa mambo mabaya katika hazina yake mbaya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtu mwema hutoa mema katika kilimbiko chake chema, lakini mtu mbaya hutoa mabaya katika kilimbiko chake kibaya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu muzuri anatwaa vitu vizuri toka ndani ya akiba yake nzuri, naye mutu mubaya anatwaa vitu vibaya toka ndani ya akiba yake mbaya.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa mema: na mtu mbaya katika hazina yake mbaya hutoa mabaya,