Matthew 12:39 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye akawajibu, “Kizazi kiovu kisicho na uaminifu! Mnataka ishara, lakini hamtapewa ishara isipokuwa ile ishara ya nabii Yona.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini yeye akawajibu, “Kizazi kiovu na cha uzinzi kinaomba ishara! Lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ile ishara ya nabii Yona.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akajibu, “Watu wenye dhambi na wasio na imani hutafuta kuona muujiza kama ishara kutoka kwa Mungu. Lakini hakuna muujiza utakaofanyika kudhibitisha chochote kwao. Yona ni ishara pekee itakayotolewa kwenu ninyi mlio wa kizazi kiovu cha leo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naye akawajibu, “Kizazi kiovu kisicho na uaminifu! Mnataka ishara; hamtapewa ishara nyingine, ila tu ile ishara ya nabii Yona.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye akawajibu, “Kizazi kiovu kisicho na uaminifu! Mnataka ishara, lakini hamtapewa ishara isipokuwa ile ishara ya nabii Yona.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini yeye akawajibu, “Kizazi kiovu na cha uzinzi kinaomba ishara! Lakini hakitapewa ishara yo yote isipokuwa ile ishara ya nabii Yona.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini yeye akawajibu, “Kizazi kiovu na cha uzinzi kinaomba ishara! Lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ile ishara ya nabii Yona.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye akawajibu, “Kizazi kiovu kisicho na uaminifu! Mnataka ishara, lakini hamtapewa ishara isipokuwa ile ishara ya nabii Yona.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye akajibu akiwaambia: Wao wa ukoo huu mbaya wenye ugoni wanatafuta kielekezo, lakini hawatapata kielekezo, ila kielekezo cha mfumbuaji Yona.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akawajibu: “Watu wa kizazi kibaya na kinachokosa uaminifu mbele ya Mungu, wanataka kuona kitambulisho. Lakini hawataona kitambulisho isipokuwa kitambulisho cha nabii Yona.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zina chataka ishara, wala hakitapewa ishara, ilia ishara ya nabii Yunus.