Matthew 12:4 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yeye aliingia katika nyumba ya Mungu akala ile mikate iliyowekwa mbele ya Mungu. Yeye wala hao wenzake hawakuruhusiwa kula mikate hiyo isipokuwa tu makuhani peke yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Aliingia katika nyumba ya Mungu, akala mikate iliyowekwa wakfu, yeye na wenzake, jambo ambalo halikuwa halali kwao kufanya, isipokuwa makuhani tu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaila mikate ile ya wonyesho, ambayo si halali kwake kuila wala kwa wale wenziwe, ila kwa makuhani peke yao?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Daudi aliingia katika nyumba ya Mungu. Yeye na wale waliokuwa pamoja naye walikula mkate uliotolewa kwa Mungu. Ilikuwa kinyume cha sheria kwa Daudi au wale waliokuwa pamoja naye kula mkate huo. Makuhani pekee ndio walioruhusiwa kuula.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yeye aliingia katika Nyumba ya Mungu pamoja na wenzake, wakala ile mikate iliyowekwa mbele ya Mungu. Yeye wala hao wenzake hawakuruhusiwa kula mikate hiyo isipokuwa tu makuhani peke yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yeye aliingia katika nyumba ya Mungu akala ile mikate iliyowekwa mbele ya Mungu. Yeye wala hao wenzake hawakuruhusiwa kula mikate hiyo isipokuwa tu makuhani peke yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Aliingia katika nyumba ya Mungu akala mikate iliyowekwa wakfu, yeye na wenzake, jambo ambalo halikuwa halali kwao kufanya, isipokuwa makuhani peke yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Aliingia katika nyumba ya Mungu, akala mikate iliyowekwa wakfu, yeye na wenzake, jambo ambalo halikuwa halali kwao kufanya, isipokuwa makuhani peke yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaila mikate ile ya wonesho, ambayo si halali kwake kuila wala kwa wale wenziwe, ila kwa makuhani peke yao?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yeye aliingia katika nyumba ya Mungu akala ile mikate iliyowekwa mbele ya Mungu. Yeye wala hao wenzake hawakuruhusiwa kula mikate hiyo isipokuwa tu makuhani peke yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo aliingia Nyumbani mwa Mungu, wakaila mikate aliyowekewa Bwana, nayo kuila ni mwiko kwake na kwa wenziwe, huliwa na watambikaji peke yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaila mikate ile ya wonyesho, ambayo si halali kwake kuila wala kwa wale wenziwe, ila kwa makuhani peke yao?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Aliingia ndani ya nyumba ya Mungu na kula mikate mitakatifu iliyotolewa kwa Mungu. Ijapokuwa vile haikuruhusiwa kwake wala kwa watu wake kukula mikate kama ile, isipokuwa makuhani peke yao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaila mikate iliyotolewa kwa Mungu, isiyo halali kuliwa nae wala na wenzi wake, illa na makuhani peke yao?