Matthew 12:42 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Malkia wa kusini atatokea wakati kizazi hiki kitakapohukumiwa, naye atakihukumu kwamba kina hatia. Maana yeye alisafiri kutoka mbali, akaja kusikiliza maneno ya hekima ya Solomoni, na kumbe hapa kuna kikuu kuliko Solomoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Malkia wa Kusini atasimama wakati wa hukumu na kukihukumu kizazi hiki. Kwa kuwa yeye alikuja kutoka miisho ya dunia ili kuisikiliza hekima ya Sulemani. Na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Malkia wa kusini atasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu yeye alikuja kutoka pande za mwisho za dunia ili asikie hekima ya Sulemani, na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Pia, siku ya hukumu, Malkia wa Kusini atasimama pamoja na wale wanaoishi sasa, atasababisha mhukumiwe kuwa na makosa. Ninasema hivi kwa sababu alisafiri kutoka mbali, mbali sana kuja kusikiliza mafundisho yenye hekima ya Sulemani. Nami Ninawaambia aliye mkuu zaidi ya Sulemani yuko hapa, lakini hamnisikii!
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Malkia wa kusini atatokea wakati kizazi hiki kitakapohukumiwa, naye atakihukumu kwamba kina hatia. Maana yeye alisafiri kutoka mbali akaja kusikiliza maneno ya hekima ya Solomoni, na kumbe hapa kuna kikuu kuliko Solomoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Malkia wa kusini atatokea wakati kizazi hiki kitakapohukumiwa, naye atakihukumu kwamba kina hatia. Maana yeye alisafiri kutoka mbali, akaja kusikiliza maneno ya hekima ya Solomoni, na kumbe hapa kuna kikuu kuliko Solomoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Malkia wa Kusini atasimama wakati wa hukumu na kukihukumu kizazi hiki, kwa kuwa yeye alikuja kutoka miisho ya dunia ili kuisikiliza hekima ya Solomoni na hapa yupo aliye mkuu kuliko Solomoni.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Malkia wa Kusini atasimama wakati wa hukumu na kukihukumu kizazi hiki. Kwa kuwa yeye alikuja kutoka miisho ya dunia ili kuisikiliza hekima ya Sulemani. Na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Malkia wa kusini atasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu yeye alikuja kutoka pande za mwisho za dunia ili asikie hekima ya Sulemani, na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Malkia wa kusini atatokea wakati kizazi hiki kitakapohukumiwa, naye atakihukumu kwamba kina hatia. Maana yeye alisafiri kutoka mbali, akaja kusikiliza maneno ya hekima ya Solomoni, na kumbe hapa kuna kikuu kuliko Solomoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yule mfalme wa kike aliyetoka kusini atauinukia ukoo huu siku ya hukumu auumbue. Kwani yeye alitoka mapeoni kwa nchi, aje kuusikia werevu wa Salomo uliokuwa wa kweli. Tena tazameni, hapa yupo anayempita Salomo!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Malkia wa kusini atasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu yeye alikuja kutoka pande za mwisho za dunia ili asikie hekima ya Sulemani, na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile kwa Siku ya hukumu malkia toka kusini atasimama na watu wa kizazi hiki na kuwashitaki, kwa sababu yeye alitoka mbali sana kuja kusikia maneno ya hekima ya mufalme Solomono. Hapa kuna yule anayekuwa mukubwa kumupita Solomono!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Malkia wa kusini ataondoka siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nae atakihukumu: maana yeye alikuja kutoka pande za mwisho za ulimwengu asikie hekima ya Sulemani; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.