Matthew 12:45 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
huenda kuwachukua pepo wengine saba, wabaya kuliko yeye; na wote huja wakamwingia huyo mtu. Na hali ya mtu huyo sasa huwa mbaya kuliko hapo mwanzo. Ndivyo itakavyokuwa kwa watu hawa waovu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha huenda na kuwaleta pepo wachafu wengine saba wabaya kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo. Nayo hali ya mwisho ya yule mtu huwa ni mbaya kuliko ile ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kiovu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
hutoka nje na kuleta roho zingine saba zilizo chafu zaidi yake. Huingia na kuishi humo, na mtu huyo anakuwa na matatizo mengi kuliko mwanzo wakati roho chafu moja iliishi ndani yake. Ndivyo ilivyo kwa kizazi hiki cha watu wanaoishi leo.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
huenda kuwachukua pepo wengine saba, wabaya kuliko yeye; na wote huja wakamwingia huyo mtu. Na hali ya mtu huyo sasa huwa mbaya kuliko hapo mwanzo. Ndivyo itakavyokuwa kwa watu hawa waovu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
huenda kuwachukua pepo wengine saba, wabaya kuliko yeye; na wote huja wakamwingia huyo mtu. Na hali ya mtu huyo sasa huwa mbaya kuliko hapo mwanzo. Ndivyo itakavyokuwa kwa watu hawa waovu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha huenda na kuwaleta pepo wachafu wengine saba, wabaya zaidi kuliko yeye, nao huingia na kuishi humo. Nayo hali ya mwisho ya mtu yule huwa mbaya zaidi kuliko ile ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki cha uovu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha huenda na kuwaleta pepo wachafu wengine saba wabaya kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo. Nayo hali ya mwisho ya yule mtu huwa ni mbaya kuliko ile ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kiovu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
huenda kuwachukua pepo wengine saba, wabaya kuliko yeye; na wote huja wakamwingia huyo mtu. Na hali ya mtu huyo sasa huwa mbaya kuliko hapo mwanzo. Ndivyo itakavyokuwa kwa watu hawa waovu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ndipo, anapokwenda kuchukua pepo saba wengine walio wabaya kuliko yeye, wawe wenziwe; nao huingia, wakae humo: hivyo ya mwisho ya mtu yule yatakuwa mabaya kuliko ya kwanza. Ndivyo, vitakavyowapata wao wa ukoo huu ulio mbaya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu anakwenda kutwaa pepo wengine saba wanaokuwa wabaya kumupita, nao wote wanakuja kuingia na kukaa mule. Na hali ya mwisho ya mutu yule inageuka mbaya kuliko hali yake ya kwanza. Na hivi ndivyo itakavyokuwa kwa watu wa kizazi hiki kibaya.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Marra huenda, akachukua pamoja nae pepo wengine saba walio waovu kupita nafsi yake, nao huingia na kukaa humo; na mambo, ya mwisho ya mtu yule huwa mabaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kiovu.