Matthew 12:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama tu mngejua maana ya maneno haya: ‘Nataka huruma wala si tambiko,’ hamngewahukumu watu wasio na hatia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama mngekuwa mmejua maana ya maneno haya, ‘Nataka rehema, wala si dhabihu,’ msingewalaumu watu wasio na hatia,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini kama mngalijua maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka, msingaliwalaumu wasio na hatia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Maandiko yanasema, ‘Sihitaji dhabihu ya wanyama; Ninataka ninyi muoneshe wema kwa watu.’ Hakika hamjui hilo linamaanisha nini. Iwapo mngelielewa, msingewahukumu wale ambao hawajafanya chochote kibaya.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kama tu mngejua maana ya maneno haya: Nataka huruma wala si dhabihu, hamngewahukumu watu wasio na hatia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama tu mngejua maana ya maneno haya: ‘Nataka huruma wala si tambiko,’ hamngewahukumu watu wasio na hatia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama mngelikuwa mmejua maana ya maneno haya, ‘Ninataka rehema, wala si dhabihu,’ msingeliwalaumu watu wasio na hatia,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama mngekuwa mmejua maana ya maneno haya, ‘Nataka rehema, wala si dhabihu,’ msingewalaumu watu wasio na hatia,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini kama mngalijua maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka, msingaliwalaumu wasio na hatia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama tu mngejua maana ya maneno haya: ‘Nataka huruma wala si tambiko,’ hamngewahukumu watu wasio na hatia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kama mngalitambua maana ya neno la kwamba: Huruma ndizo, nizitakazo, lakini vipaji vya tambiko sivyo, basi, hamngaliwawazia mabaya wasio na kosa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini kama mngalijua maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka, msingaliwalaumu wasio na hatia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungejua maana ya Maandiko haya Matakatifu, yanayosema: ‘Ninataka huruma, lakini si sadaka zenu,’ hamungehukumu watu hawa wasiokuwa na kosa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kama mngalijua maana ya maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka, hamngaliwalaumu wasio na khatiya.