Matthew 13:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana, aliye na kitu atapewa na kuzidishiwa; lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana yule aliye na kitu atapewa zaidi, naye atakuwa navyo tele. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana ye yote mwenye kitu atapewa, naye atazidishiwa tele; lakini ye yote asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha akawaambia, ‘Zingatieni kwa makini kile mnachokisikia. Kwani jinsi mnavyosikiliza kwa makini, ndivyo mtakavyoelewa na kuzidi kuelewa. Kwa kuwa kila aliye na uelewa kidogo ataongezewa zaidi. Lakini wale wasiosikiliza kwa makini watapoteza hata ule uelewa mdogo walio nao.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana, aliye na kitu atapewa na kuzidishiwa; lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana, aliye na kitu atapewa na kuzidishiwa; lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana yule aliye na kitu atapewa zaidi, naye atakuwa navyo tele, lakini yule asiye na kitu, hata kile alichonacho atanyang'anywa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana yule aliye na kitu atapewa zaidi, naye atakuwa navyo tele. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana yeyote mwenye kitu atapewa, naye atazidishiwa tele; lakini yeyote asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana, aliye na kitu atapewa na kuzidishiwa; lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
lakini wale hawakupewa. Kwani ye yote aliye na mali atapewa, ziwe nyingi zaidi; lakini asiye na kitu atachukuliwa hata kile, alicho nacho.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana ye yote mwenye kitu atapewa, naye atazidishiwa tele; lakini ye yote asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana mutu anayekuwa na kitu ataongezewa kingine, naye atakuwa na vitu vingi. Lakini mutu asiyekuwa na kitu, ataondolewa hata kile kidogo anachokuwa nacho.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana ye yote aliye na mali atapewa, na hado atazidishiwa tele: lakini ye yote asiye nayo, hatta ile aliyo nayo ataondolewa.