Matthew 13:15 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana akili za watu hawa zimepumbaa, wameyaziba masikio yao, wameyafumba macho yao. La sivyo, wangeona kwa macho yao, wangesikia kwa masikio yao, wangeelewa kwa akili zao, na kunigeukia, asema Bwana, nami ningewaponya.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa mioyo ya watu hawa imekuwa migumu; hawasikii kwa masikio yao, na wamefumba macho yao. Wasije wakaona kwa macho yao, na wakasikiliza kwa masikio yao, wakaelewa kwa mioyo yao, na kugeuka nami nikawaponya.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndiyo, akili za watu hawa sasa zimefungwa. Wana masikio, lakini hawasikii vizuri. Wana macho, lakini wameyafumba. Iwapo akili zao zisingekuwa zimefungwa, wangeona kwa macho yao; wangesikia kwa masikio yao; Iwapo wangeelewa kwa akili zao. Kisha wangenigeukia na kuponywa.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana akili za watu hawa zimepumbaa, wameyaziba masikio yao, wameyafumba macho yao. La sivyo, wangeona kwa macho yao. wangesikia kwa masikio yao, wangeelewa kwa akili zao, na kunigeukia, asema Bwana, nami ningewaponya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana akili za watu hawa zimepumbaa, wameyaziba masikio yao, wameyafumba macho yao. La sivyo, wangeona kwa macho yao, wangesikia kwa masikio yao, wangeelewa kwa akili zao, na kunigeukia, asema Bwana, nami ningewaponya.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, hawasikii kwa masikio yao, na wamefumba macho yao. Wasije wakaona kwa macho yao, wakasikia kwa masikio yao, wakaelewa kwa mioyo yao, wakageuka, nami nikawaponya.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa mioyo ya watu hawa imekuwa migumu; hawasikii kwa masikio yao, na wamefumba macho yao. Wasije wakaona kwa macho yao, na wakasikiliza kwa masikio yao, wakaelewa kwa mioyo yao, na kugeuka nami nikawaponya.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana akili za watu hawa zimepumbaa, wameyaziba masikio yao, wameyafumba macho yao. La sivyo, wangeona kwa macho yao, wangesikia kwa masikio yao, wangeelewa kwa akili zao, na kunigeukia, asema Bwana, nami ningewaponya.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mioyo yao walio ukoo huu imeshupazwa, hata kwa masikio yao yaliyo mazito hawasikii; nayo macho yao wameyasinziza, wasije wakaona kwa macho, au wakasikia kwa masikio, au wakajua maana kwa mioyo, wakanigeukia, nikawaponya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana mioyo ya watu hawa imegeuka migumu, wameziba masikio yao, nao wamefunga macho yao, kusudi wasipate kuona, nao wasipate kusikia, wala wasipate kunigeukia, nami ningewaponyesha.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana moyo wa watu hawa umekuwa mzito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao Wakasikia kwa masikio yao, Wakafahama kwa mioyo yao, Wakaongoka, Nikawaponya.