Matthew 13:2 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Makundi makubwa ya watu yalimzunguka hata Yesu akapanda mashuani, akaketi. Watu wote walisimama kwenye ukingo wa ziwa,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Umati mkubwa mno wa watu wakakusanyika kumzunguka, hata ikabidi aingie katika chombo na kuketi humo, nao watu wote wakawa wamesimama ukingoni mwa bahari.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakamkusanyikia makutano mengi, hata akapanda chomboni, akaketi; na ule mkutano wote wakasimama pwani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kundi kubwa wakakusanyika kumzunguka. Hivyo akapanda mtumbwini na kuketi. Watu wote wakabaki ufukweni.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Makundi makubwa ya watu yalimzunguka hata Yesu akapanda mashua, akaketi. Hao watu walisimama kwenye ukingo wa ziwa,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Makundi makubwa ya watu yalimzunguka hata Yesu akapanda mashuani, akaketi. Watu wote walisimama kwenye ukingo wa ziwa,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Umati mkubwa mno wa watu ukakusanyika kumzunguka hata ikabidi aingie katika chombo na kuketi humo, nao watu wote wakawa wamesimama ukingoni mwa bahari.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Umati mkubwa mno wa watu ukakusanyika kumzunguka, hata ikabidi aingie katika chombo na kuketi humo, nao watu wote wakawa wamesimama ukingoni mwa bahari.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakamkusanyikia makutano mengi, hata akapanda katika mashua, akaketi; na ule mkutano wote wakasimama pwani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Makundi makubwa ya watu yalimzunguka hata Yesu akapanda mashuani, akaketi. Watu wote walisimama kwenye ukingo wa ziwa,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakamkutanyikia makundi mengi ya watu, kwa hiyo akaingia chomboni, akakaa humo, watu wote wakisimama pwani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakamkusanyikia makutano mengi, hata akapanda chomboni, akaketi; na ule mkutano wote wakasimama pwani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kuona kundi kubwa la watu waliokusanyika karibu naye, akapanda ndani ya chombo na kukaa humo, nao watu walibaki wakisimama inchi kavu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakamkusanyikia watu wengi, hatta akapanda chomboni, akaketi; na mkutano wote wakasimama pwani.