Matthew 13:22 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ile mbegu iliyoanguka kati ya miti ya miiba, ni mfano wa mtu asikiaye hilo neno, lakini wasiwasi wa ulimwengu huu na anasa za mali hulisonga neno hilo, naye hazai matunda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ile mbegu iliyopandwa katika miiba ni yule mtu anayelisikia neno, lakini masumbufu ya maisha haya na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno na kulifanya lisizae matunda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye aliyepandwa penye miiba, huyo ndiye alisikiaye lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno; likawa halizai.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na vipi kuhusu mbegu zilizoanguka katikati ya miiba? Hizo zinafanana na watu wanaosikia mafundisho lakini huyaruhusu mahangaiko ya maisha na kutaka utajiri, hufanya mafundisho yasikue. Hivyo mafundisho hayazai mazao mazuri katika maisha yao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ile mbegu iliyoanguka kati ya miti ya miiba, ni mfano wa mtu asikiaye huo ujumbe, lakini wasiwasi wa ulimwengu huu na anasa za mali huusonga ujumbe huo, naye hazai matunda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ile mbegu iliyoanguka kati ya miti ya miiba, ni mfano wa mtu asikiaye hilo neno, lakini wasiwasi wa ulimwengu huu na anasa za mali hulisonga neno hilo, naye hazai matunda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ile mbegu iliyopandwa katika miiba ni yule mtu alisikiaye neno, lakini masumbufu ya dunia na ushawishi wa mali hulisonga lile neno na kulifanya lisizae matunda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ile mbegu iliyopandwa katika miiba ni yule mtu alisikiaye neno, lakini masumbufu ya maisha haya na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno na kulifanya lisizae matunda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye aliyepandwa penye miiba, huyo ndiye alisikiaye lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno; likawa halizai.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ile mbegu iliyoanguka kati ya miti ya miiba, ni mfano wa mtu asikiaye hilo neno, lakini wasiwasi wa ulimwengu huu na anasa za mali hulisonga neno hilo, naye hazai matunda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini zilizomiagwa penye miiba ni kama mtu anayelisikia Neno, lakini masumbuko ya dunia hii na udanganyifu wa mali hulisonga Neno, lisizae matunda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye aliyepandwa penye miiba, huyo ndiye alisikiaye lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno; likawa halizai.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Pahali zile mbegu zilipoanguka katika miiba, ni mufano wa wale wanaosikia Neno la Mungu, lakini masumbuko ya dunia hii na udanganyifu wa mali vinasonga lile neno linalokuwa ndani yao na kulizuiza kuzaa matunda.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nae aliyepandwa penye miiba, huyu ndiye alisikiae lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno, likawa halizai.