Matthew 13:32 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yenyewe ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini ikisha ota huwa kubwa kuliko mimea yote. Hukua ikawa mti, hata ndege wa angani huja na kujenga viota katika matawi yake.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ingawa mbegu hiyo ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini inapokua ni mmea mkubwa kuliko yote ya bustanini, nao huwa mti mkubwa, hadi ndege wa angani wanakuja na kutengeneza viota katika matawi yake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nayo ni ndogo kuliko mbegu zote; lakini ikiisha kumea, huwa kubwa kuliko mboga zote, ikawa mti, hata nyuni wa angani huja na kukaa katika matawi yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ni mbegu ndogo sana kuliko mbegu zote. Lakini unapokua, ni kubwa kuliko mimea yote ya bustanini. Unakuwa mti mkubwa unaotosha ndege kuja na kutengeneza viota kwenye matawi yake.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yenyewe ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini ikishaota huwa kubwa kuliko mimea yote. Hukua ikawa mti, na ndege wa angani huja na kujenga viota katika matawi yake.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yenyewe ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini ikisha ota huwa kubwa kuliko mimea yote. Hukua ikawa mti, hata ndege wa angani huja na kujenga viota katika matawi yake.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ingawa mbegu hiyo ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini inapokua ni mmea mkubwa kuliko yote ya bustanini, nao huwa mti mkubwa, hata ndege wa angani huja na kutengeneza viota katika matawi yake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ingawa mbegu hiyo ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini inapokua ni mmea mkubwa kuliko yote ya bustanini, nao huwa mti mkubwa, hadi ndege wa angani wanakuja na kutengeneza viota katika matawi yake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nayo ni ndogo kuliko mbegu zote; lakini ikiisha kumea, huwa kubwa kuliko miboga yote ikawa mti, hata ndege wa angani huja na kukaa katika matawi yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yenyewe ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini ikisha ota huwa kubwa kuliko mimea yote. Hukua ikawa mti, hata ndege wa angani huja na kujenga viota katika matawi yake.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nacho ni kidogo kuliko mbegu zote. Lakini kinapokua ni mkubwa kuliko miboga yote inayopandwa, huwa mti mzima, hata ndege wa angani huja na kutua katika matawi yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nayo ni ndogo kuliko mbegu zote; lakini ikiisha kumea, huwa kubwa kuliko mboga zote, ikawa mti, hata nyuni wa angani huja na kukaa katika matawi yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mbegu hii ni ndogo sana kuliko mbegu zote, lakini inapokwisha kuota, inakuwa kubwa zaidi kuliko mimea yote, hata ndege wanakuja na kujenga chicha zao katikati ya matawi yake.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
nayo ni ndogo kuliko mbegu zote; lakini ikiisha kumea, ni kubwa kuliko mboga zote, ikawa mti, hatta ndege za anga huja na kutua katika matawi yake.