Matthew 13:34 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu aliwaambia watu hayo yote kwa mifano. Hakuwaambia chochote bila kutumia mifano,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa alinena mambo haya yote kwa umati wa watu kwa mifano, wala hakuwaambia lolote pasipo mfano.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hayo yote Yesu aliwaambia makutano kwa mifano; wala pasipo mfano hakuwaambia neno;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu alitumia simulizi akasema mambo yote haya kwa watu. Daima alitumia simulizi kuwafundisha.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu aliwaambia watu hayo yote kwa mifano. Hakuwaambia chochote bila kutumia mifano,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu aliwaambia watu hayo yote kwa mifano. Hakuwaambia chochote bila kutumia mifano,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu alinena mambo haya yote kwa makutano kwa mifano. Wala pasipo mfano hakuwaambia lo lote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa alinena mambo haya yote kwa makutano kwa mifano. Wala hakuwaambia lolote pasipo mfano.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hayo yote Yesu aliwaambia makutano kwa mifano; wala pasipo mfano hakuwaambia neno;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu aliwaambia watu hayo yote kwa mifano. Hakuwaambia chochote bila kutumia mifano,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Haya yote aliwaambia makundi ya watu kwa mifano, pasipo mfano hakuwaambia neno,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hayo yote Yesu aliwaambia makutano kwa mifano; wala pasipo mfano hakuwaambia neno;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu aliwaambia makundi ya watu maneno hayo yote akitumia mifano. Yeye hakusema nao pasipo kutumia mifano.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Haya yote Yesu aliwaambia makutano kwa mifano; na pasipo mfano hakuwaambia neno: