Matthew 13:35 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
ili jambo lililonenwa na nabii litimie: “Nitasema nao kwa mifano; nitafichua yaliyofichika tangu kuumbwa ulimwengu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hii ilikuwa ili kutimiza neno lililonenwa na nabii, aliposema: “Nitafungua kinywa changu niseme nao kwa mifano; nitahubiri mambo yaliyofichika tangu kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema, Nitafumbua kinywa changu kwa mifano, Nitayatamka yaliyositirika tangu awali.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hii ilikuwa kuweka wazi maana halisi kama manabii walivyosema: “Nitazungumza kwa kutumia simulizi; Nitayasema mambo ambayo yamekuwa siri tangu ulimwengu ulipoumbwa.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
ili jambo lililonenwa na nabii litimie: “Nitasema kwa mifano; nitawaambia mambo yaliyofichika tangu kuumbwa ulimwengu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
ili jambo lililonenwa na nabii litimie: “Nitasema nao kwa mifano; nitafichua yaliyofichika tangu kuumbwa ulimwengu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hii ilikuwa ili kutimiza lile lililonenwa kwa vinywa vya manabii kusema: “Nitakifungua kinywa changu niseme nao kwa mifano, nitahubiri mambo yaliyofichika tangu kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hii ilikuwa ili kutimiza lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii aliposema: “Nitafungua kinywa changu niseme nao kwa mifano; nitahubiri mambo yaliyofichika tangu kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema, Nitafumbua kinywa changu kwa mifano, Nitayatamka yaliyositirika tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
ili jambo lililonenwa na nabii litimie: “Nitasema nao kwa mifano; nitafichua yaliyofichika tangu kuumbwa ulimwengu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kusudi litimie lililosemwa na mfumbuaji, akisema: Nitakifumbua kinywa changu, kiseme mifano. Nitatangaza mambo yaliyofichika tangu hapo, ulimwengu ulipoumbwa.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema, Nitafumbua kinywa changu kwa mifano, Nitayatamka yaliyositirika tangu awali.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ilitokea vile kusudi yatimie maneno yaliyosemwa kwa njia ya nabii: “Nitasema nao kwa mifano, nitawaambia maneno yaliyofichwa tangu kuumbwa kwa dunia.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
illi litimizwe neno lililonenwa mi nabii, akisema, Nitafunua kinywa changu kwa mifano, Nitatoa mambo yaliyostirika tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu.