Matthew 13:4 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alipokuwa akipanda mbegu, nyingine zilianguka njiani, ndege wakaja wakazila.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipokuwa akitawanya mbegu, nyingine zilianguka kando ya njia, nao ndege wakaja na kuzila.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata alipokuwa akipanda, mbegu nyingine zilianguka karibu na njia, ndege wakaja wakazila;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alipokuwa anatawanya mbegu, baadhi ziliangukia njiani. Ndege wakaja na kuzila zote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Alipokuwa akipanda, nyingine zilianguka njiani, ndege wakaja wakazila.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alipokuwa akipanda mbegu, nyingine zilianguka njiani, ndege wakaja wakazila.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipokuwa akipanda, baadhi zikaanguka kando ya njia, ndege wakaja na kuzila.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipokuwa akitawanya mbegu, nyingine zilianguka kando ya njia, nao ndege wakaja na kuzila.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na alipokuwa akipanda, mbegu nyingine zilianguka karibu na njia, ndege wakaja wakazila;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alipokuwa akipanda mbegu, nyingine zilianguka njiani, ndege wakaja wakazila.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa alipozimiaga, nyingine zikaangukia njiani; ndege wakaja, wakazila.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata alipokuwa akipanda, mbegu nyingine zilianguka karibu na njia, ndege wakaja wakazila;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alipokuwa akipanda mbegu katika shamba lake, zimoja zikaanguka pembeni ya njia, nao ndege wakakuja na kuzikula.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta alipokuwa akipanda, nyingine zikaanguka njiani, ndege wakaja wakazila: