Matthew 13:44 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ufalme wa mbinguni unafanana na hazina iliyofichika shambani. Mtu mmoja aliigundua, akaificha tena. Alifurahi sana hata akaenda kuuza yote aliyokuwa nayo, akalinunua shamba lile.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ufalme wa mbinguni unafanana na hazina iliyofichwa shambani, ambayo mtu mmoja alipoiona akaificha tena. Kisha katika furaha yake, akaenda akauza vyote alivyokuwa navyo, akalinunua lile shamba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ufalme wa Mungu unafanana na hazina iliyofichwa shambani. Siku moja mtu alipoiona aliificha tena; na kwa sababu alikuwa na furaha sana alikwenda kuuza kila kitu alichonacho na kulinunua shamba.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyofichika shambani. Mtu mmoja aliigundua, akaificha tena. Alifurahi sana hata akaenda kuuza yote aliyokuwa nayo, akalinunua shamba lile.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ufalme wa mbinguni unafanana na hazina iliyofichika shambani. Mtu mmoja aliigundua, akaificha tena. Alifurahi sana hata akaenda kuuza yote aliyokuwa nayo, akalinunua shamba lile.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ufalme wa Mbinguni unafanana na hazina iliyofichwa shambani, ambayo mtu mmoja alipoiona akaificha tena. Kisha katika furaha yake, akaenda akauza vyote alivyokuwa navyo, akalinunua lile shamba.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ufalme wa Mbinguni unafanana na hazina iliyofichwa shambani, ambayo mtu mmoja alipoiona akaificha tena. Kisha katika furaha yake, akaenda akauza vyote alivyokuwa navyo, akalinunua lile shamba.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Ufalme wa mbinguni unafanana na hazina iliyofichika shambani. Mtu mmoja aliigundua, akaificha tena. Alifurahi sana hata akaenda kuuza yote aliyokuwa nayo, akalinunua shamba lile.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Ufalme wa mbingu umefanana na fedha zilizofukiwa shambani. Mtu alipoziona akazifukia, akaenda kwa furaha yake, akaviuza vyote, alivyokuwa navyo, akalinunua shamba lile.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Ufalme wa mbinguni unafanana na mali iliyofichwa katika shamba moja. Mutu mumoja alipoiona, akaificha tena. Halafu kwa furaha kubwa akaenda kuuzisha vitu vyake vyote na kununua lile shamba.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyostirika katika shamba; mtu akaiona, akaificha; na kwa furaha yake akaenda akanza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile.