Matthew 13:54 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
akaenda kijijini kwake. Huko akawa anawafundisha watu katika sunagogi lao hata wakashangaa, wakasema, “Huyu amepata wapi hekima hii na maajabu?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipofika mji wa kwao, akawafundisha watu katika sinagogi lao. Nao wakastaajabu, wakauliza, “Mtu huyu amepata wapi hekima hii na uwezo huu wa kufanya miujiza?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na alipofika nchi yake, akawafundisha katika sinagogi lao, hata wakashangaa, wakasema, Huyu amepata wapi hekima hii na miujiza hii?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alikwenda katika mji wa kwao. Aliwafundisha watu katika sinagogi lao, nao walishangaa. Walisema, “Mtu huyu alipata wapi hekima na nguvu hii ya kutenda miujiza?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
akaenda kijijini kwake. Huko akawa anawafundisha watu katika sunagogi hata wakashangaa, wakasema, “Huyu amepata wapi hekima hii na maajabu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
akaenda kijijini kwake. Huko akawa anawafundisha watu katika sunagogi lao hata wakashangaa, wakasema, “Huyu amepata wapi hekima hii na maajabu?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipofika mjini kwao, akawafundisha watu katika sinagogi lao. Nao wakastaajabu, wakauliza, “Mtu huyu amepata wapi hekima hii na uwezo huu wa kufanya miujiza?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipofika mji wa kwao, akawafundisha watu katika sinagogi lao. Nao wakastaajabu, wakauliza, “Mtu huyu amepata wapi hekima hii na uwezo huu wa kufanya miujiza?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na alipofika mji wa kwao, akawafundisha katika sinagogi lao, hata wakashangaa, wakasema, Huyu amepata wapi hekima hii na miujiza hii?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
akaenda kijijini kwake. Huko akawa anawafundisha watu katika sunagogi lao hata wakashangaa, wakasema, “Huyu amepata wapi hekima hii na maajabu?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipofika kwao, alikokulia, akawafundisha katika nyumba yao ya kuombea, nao wakashangaa wakisema: Huyu amepata wapi werevu huu ulio wa kweli na nguvu hizi?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na alipofika nchi yake, akawafundisha katika sinagogi lao, hata wakashangaa, wakasema, Huyu amepata wapi hekima hii na miujiza hii?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
na kwenda katika muji wake mwenyewe. Kule akaanza kuwafundisha watu katika nyumba zao za kuabudia, nao walishangaa na kuuliza: “Huyu amepata hekima na miujiza hii kutoka wapi?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na alipofika inchi yake, akawafundisha katika sunagogi yao, hatta wakashangaa, wakanena, Huyu amepata wapi hekima hii na miujiza hii?