Matthew 14:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wanafunzi wa Yohane wakaja, wakauchukua mwili wake, wakauzika. Kisha wakaenda kumpasha habari Yesu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanafunzi wa Yahya wakaja na kuuchukua mwili wake, wakamzika. Kisha wakaenda wakamwambia Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wanafunzi wake wakaenda, wakamchukua yule maiti, wakamzika; kisha wakaenda wakampasha Yesu habari.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wafuasi wa Yohana wakaja na kuuchukua mwili wa Yohana na kuuzika. Kisha wakaenda na kumwambia Yesu kilichotokea.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wanafunzi wa Yohane wakaja, wakauchukua mwili wake, wakauzika. Kisha wakaenda kumpasha habari Yesu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wanafunzi wa Yohane wakaja, wakauchukua mwili wake, wakauzika. Kisha wakaenda kumpasha habari Yesu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wanafunzi wa Yohana wakaja na kuuchukua mwili wake kwenda kuuzika. Kisha wakaenda wakamwambia Yesu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wanafunzi wa Yahya wakaja na kuuchukua mwili wake kwenda kuuzika. Kisha wakaenda wakamwambia Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wanafunzi wake wakaenda, wakamchukua yule maiti, wakamzika; kisha wakaenda wakampasha Yesu habari.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wanafunzi wa Yohane wakaja, wakauchukua mwili wake, wakauzika. Kisha wakaenda kumpasha habari Yesu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wanafunzi wake wakaja, wakautwaa mwili wake, wakauzika; kisha wakaenda, wakampasha Yesu habari.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wanafunzi wake wakaenda, wakamchukua yule maiti, wakamzika; kisha wakaenda wakampasha Yesu habari.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wanafunzi wa Yoane wakakuja kubeba maiti yake na kuizika. Nao wakaenda kumwelezea Yesu habari ile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wanafunzi wake wakaenda, wakauchukua mwili wake, wakauzika; wakaenda wakampasha Yesu khabari.