Matthew 14:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na saa za mchana zimepita. Basi, uwaage watu ili waende vijijini wakajinunulie chakula.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ilipofika jioni, wanafunzi wake walienda kwake, wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na muda sasa umekwisha. Waage makundi ya watu ili waende zao vijijini wakajinunulie chakula.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na saa imekwisha pita; uwaage makutano, waende zao vijijini, wakajinunulie vyakula.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baadaye mchana huo, wafuasi walimwendea Yesu na kusema, “Hakuna anayeishi katika eneo hili. Na tayari muda umepita, hivyo waage watu ili waende katika miji na kujinunulia chakula.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na saa zimepita. Basi, uwaage watu ili waende vijijini wakajinunulie chakula.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na saa za mchana zimepita. Basi, uwaage watu ili waende vijijini wakajinunulie chakula.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ilipofika jioni, wanafunzi wake wakamjia wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na muda sasa umekwisha, waage makutano ili waende zao vijijini wakajinunulie chakula.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ilipofika jioni, wanafunzi wake walienda kwake, wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na muda sasa umekwisha. Waage makutano ili waende zao vijijini wakajinunulie chakula.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na saa imekwisha pita; uwaage makutano, waende zao vijijini, wakajinunulie vyakula.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na saa za mchana zimepita. Basi, uwaage watu ili waende vijijini wakajinunulie chakula.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ilipokuwa jioni, wanafunzi wake wakamjia, wakasema: Hapa tulipo ni nyika, nazo saa za mchana zimepita; basi, waage hawa watu wengi, waende zao vijijini, wajinunulie vyakula!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na saa imekwisha pita; uwaage makutano, waende zao vijijini, wakajinunulie vyakula.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na ilipokuwa magaribi, wanafunzi wake wakamufikia na kumwambia: “Hapa ni pori na sasa ni magaribi. Uage kundi hili kusudi waende katika vijiji kwa kujinunulia vyakula.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta ilipokuwa jioni, wanafunzi wake wakamwendea, wakanena, Mahali hapa nyika tupu, na saa imekwisha pita; waage makutano, waende zao vijijini, wakajinunulie vyakula.