Matthew 14:22 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mara, Yesu akawaamuru wanafunzi wake wapande mashua, wamtangulie ngambo ya ziwa wakati yeye anayaaga makundi ya watu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mara Isa akawaambia wanafunzi wake waingie katika mashua wamtangulie kwenda ng’ambo ya bahari, wakati yeye alikuwa akiaga ule umati.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mara akawalazimisha wanafunzi wake wapande chomboni na kutangulia mbele yake kwenda ng'ambo, wakati yeye alipokuwa akiwaaga mkutano.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mara baada ya hili Yesu akawaambia wafuasi wake wapande kwenye mtumbwi. Akawaambia waende upande mwingine wa ziwa. Aliwaambia angekuja baadaye, alikaa pale ili kuwaaga watu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mara, Yesu akawaamuru wanafunzi wake wapande mashua, wamtangulie ng'ambo ya ziwa wakati yeye anawaaga watu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mara, Yesu akawaamuru wanafunzi wake wapande mashua, wamtangulie ng'ambo ya ziwa wakati yeye anayaaga makundi ya watu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mara Yesu akawaambia wanafunzi wake waingie kwenye chombo watangulie kwenda ng'ambo ya pili ya bahari, wakati yeye anawaaga wale makutano.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mara Isa akawaambia wanafunzi wake waingie kwenye mashua watangulie kwenda ng’ambo ya bahari, wakati yeye alikuwa akiwaaga wale makutano.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mara akawalazimisha wanafunzi wake wapande katika mashua na kutangulia mbele yake kwenda ng'ambo, wakati yeye alipokuwa akiwaaga mkutano.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mara, Yesu akawaamuru wanafunzi wake wapande mashua, wamtangulie ngambo ya ziwa wakati yeye anayaaga makundi ya watu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Yesu akawashurutisha wanafunzi waingie chomboni, wamtangulie kwenda ng'ambo, mpaka yeye kwanza awaage makundi ya watu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mara akawalazimisha wanafunzi wake wapande chomboni na kutangulia mbele yake kwenda ng’ambo, wakati yeye alipokuwa akiwaaga mkutano.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mara moja kisha mambo hayo, Yesu akawalazimisha wanafunzi wake waingie ndani ya chombo na kumutangulia ngambo ingine ya ziwa. Kwa wakati ule yeye alibaki akiaga lile kundi la watu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Marra Yesu akawalazimisha wamifunzi wake wapande chomboni na kutangulia mbele yake kwenda ngʼambu, wakati yeye alipokuwa akiwaaga makutano.