Matthew 14:24 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na wakati huo ile mashua ilikwisha fika karibu katikati ya ziwa, lakini ilikumbwa na taabu kwa sababu upepo ulikuwa unaipinga.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huo ile mashua ilikuwa mbali kutoka nchi kavu ikisukwasukwa na mawimbi, kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kile chombo kimekwisha kufika katikati ya bahari, kinataabika sana na mawimbi; maana upepo ulikuwa wa mbisho.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakati huu mtumbwi ilikuwa mbali kutoka pwani. Kwa kuwa upepo ulikuwa unavuma kinyume na mtumbwi, mtumbwi ulikuwa unapata msukosuko kwa sababu ya mawimbi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
na wakati huo ile mashua ilikwishafika karibu katikati ya ziwa, lakini ilikuwa inakwenda mrama kwa sababu upepo ulikuwa unaipinga.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na wakati huo ile mashua ilikwisha fika karibu katikati ya ziwa, lakini ilikumbwa na taabu kwa sababu upepo ulikuwa unaipinga.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati huo kile chombo kilikuwa kimeshafika mbali kutoka nchi kavu kikisukwasukwa na mawimbi kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huo ile mashua ilikuwa mbali kutoka nchi kavu ikisukwasukwa na mawimbi, kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na ile mashua imekwisha kufika katikati ya bahari, inapigwa sana na mawimbi; maana upepo ulikuwa unawakabili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
na wakati huo ile mashua ilikwisha fika karibu katikati ya ziwa, lakini ilikumbwa na taabu kwa sababu upepo ulikuwa unaipinga.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nacho chombo kilikuwa kimeendelea kitambo kirefu kikahangaishwa na mawimbi, kwani upepo uliwatokea mbele.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kile chombo kimekwisha kufika katikati ya bahari, kinataabika sana na mawimbi; maana upepo ulikuwa wa mbisho.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
lakini chombo kilikuwa kimekwisha kufika mbali sana na inchi kavu, kikirushwarushwa na zoruba, kwa maana upepo ulikuwa ukitokea mbele.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na kile chombo kimekwisha kufika katikati ya bahari, kinataabika sana na mawimbi; maana upepo ulikuwa wa mbisho.