Matthew 14:29 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akasema, “Haya, njoo.” Basi, Petro akashuka kutoka ile mashua, akatembea juu ya maji, akamwendea Yesu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akamwambia, “Njoo.” Basi Petro akatoka kwenye chombo, akatembea juu ya maji kumwelekea Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akasema, “Njoo, Petro.” Kisha Petro akauacha mtumbwi na kutembea juu ya maji kumwelekea Yesu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akasema, “Haya, njoo.” Basi, Petro akashuka kutoka ile mashua, akatembea juu ya maji, akamwendea Yesu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akasema, “Haya, njoo.” Basi, Petro akashuka kutoka ile mashua, akatembea juu ya maji, akamwendea Yesu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akamwambia, “Njoo.” Basi Petro akatoka kwenye chombo, akatembea juu ya maji kumwelekea Yesu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akamwambia, “Njoo.” Basi Petro akatoka kwenye chombo, akatembea juu ya maji kumwelekea Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Njoo. Petro akashuka katika mashua, akatembea juu ya maji, ili kumwendea Yesu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akasema, “Haya, njoo.” Basi, Petro akashuka kutoka ile mashua, akatembea juu ya maji, akamwendea Yesu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipomwambia: Njoo! Petero akashuka chomboni, akaenda juu ya maji, amfikie Yesu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye Yesu akamujibu: “Kuja.” Halafu Petro akatoka ndani ya chombo, akaanza kutembea juu ya maji kumufikia Yesu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akatembea juu ya maji, illi kumwendea Yesu.