Matthew 14:30 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini alipouona ule upepo, aliogopa, akaanza kuzama; akalia kwa sauti, “Bwana, niokoe!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini alipoona upepo mkali aliingiwa na hofu, naye akaanza kuzama, akapaza sauti na kusema, “Bwana, niokoe!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Petro alipokuwa anatembea juu ya maji, aliyaona mawimbi na upepo. Aliogopa na kuanza kuzama katika maji. Akapiga kelele, “Bwana, niokoe!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini alipouona ule upepo, aliogopa, akaanza kuzama; akalia kwa sauti, “Bwana, niokoe!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini alipouona ule upepo, aliogopa, akaanza kuzama; akalia kwa sauti, “Bwana, niokoe!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini alipoona upepo mkali aliingiwa na hofu, naye akaanza kuzama, huku akipiga kelele, “Bwana, niokoe!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini alipoona upepo mkali aliingiwa na hofu, naye akaanza kuzama, huku akipiga kelele, “Bwana Isa, niokoe!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini alipouona ule upepo, aliogopa, akaanza kuzama; akalia kwa sauti, “Bwana, niokoe!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini alipotazama, upepo ulivyo na nguvu, akaogopa, akaanza kuzama majini, akapiga kelele akisema: Bwana, niokoa!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini alipoona upepo, akaogopa, na kwa vile alivyoanza kuzama ndani ya maji, akalalamika akisema: “Bwana, uniokoe!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini alipoona upepo wa nguvu, akaogopa: akaanza kuzama, akapiga yowe, akinena, Bwana, niokoe.