Matthew 15:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini mambo yatokayo kinywani hutoka moyoni, na hayo ndiyo yanayomtia mtu unajisi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kitokacho kinywani hutoka moyoni, na hiki ndicho kimtiacho mtu unajisi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini mambo mabaya ambayo watu wanasema kwa vinywa vyao hutokana na mawazo yao. Na hayo ndiyo yanayoweza kumtia mtu unajisi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini yale yatokayo kinywani hutoka moyoni, na hayo ndiyo yanayomtia mtu najisi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini mambo yatokayo kinywani hutoka moyoni, na hayo ndiyo yanayomtia mtu unajisi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kitokacho kinywani hutoka moyoni, na hiki ndicho kimtiacho mtu unajisi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kitokacho kinywani hutoka moyoni, na hiki ndicho kimtiacho mtu unajisi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini mambo yatokayo kinywani hutoka moyoni, na hayo ndiyo yanayomtia mtu unajisi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini yanayotoka kinywani mwa mtu yametoka moyoni mwake, nayo ndiyo yanayomtia mtu uchafu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini vyote vinavyotoka ndani ya kinywa ni vyenye kutoka kwanza ndani ya moyo wake, navyo vinamuchafua mutu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo najis mwana Adamu.