Matthew 15:2 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kwa nini wanafunzi wako hawajali mapokeo tuliyopokea kwa wazee wetu? Hawanawi mikono ipasavyo kabla ya kula!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mbona wanafunzi wako wanakiuka mapokeo ya wazee? Kwa maana wao hawanawi mikono yao kabla ya kula!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mbona wanafunzi wako huyahalifu mapokeo ya wazee, kwa maana hawanawi mikono walapo chakula.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
“Kwa nini wafuasi wako hawatii desturi tulizorithi kutoka kwa viongozi wetu wakuu walioishi hapo zamani? Wafuasi wako hawanawi mikono kabla ya kula!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Kwa nini wanafunzi wako hawajali mapokeo tuliyopokea kutoka kwa wazee wetu? Hawanawi mikono yao kama ipasavyo kabla ya kula!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kwa nini wanafunzi wako hawajali mapokeo tuliyopokea kwa wazee wetu? Hawanawi mikono ipasavyo kabla ya kula!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mbona wanafunzi wako wanakiuka mapokeo ya wazee waliopita? Kwa maana wao hawanawi mikono yao kabla ya kula!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mbona wanafunzi wako wanakiuka mapokeo ya wazee? Kwa maana wao hawanawi mikono yao kabla ya kula!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mbona wanafunzi wako huyavunja mapokeo ya wazee, kwa maana hawanawi mikono walapo chakula.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kwa nini wanafunzi wako hawajali mapokeo tuliyopokea kwa wazee wetu? Hawanawi mikono ipasavyo kabla ya kula!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa sababu gani wanafunzi wako hawayafuati mazoezo ya wakale? Kwani hawanawi mikono wakila chakula.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mbona wanafunzi wako huyahalifu mapokeo ya wazee, kwa maana hawanawi mikono walapo chakula.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Kwa sababu gani wanafunzi wako wanavunja desturi za babu zetu kwa kula chakula pasipo kunawa mikono?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mbona wanafunizi wako huyakhalifu mapokeo ya wazee, kwa maana hawanawi mikono walapo chakula.