Matthew 15:22 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, mama mmoja Mkanaani wa nchi hiyo alimjia, akapaza sauti: “Bwana, Mwana wa Daudi, nionee huruma! Binti yangu anasumbuliwa na pepo.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwanamke mmoja Mkanaani aliyeishi sehemu jirani na hizo akaja kwake akilia, akasema, “Nihurumie, Ee Bwana, Mwana wa Daudi! Binti yangu amepagawa na pepo mchafu, na anateseka sana.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mwanamke Mkanaani kutoka eneo hilo akatokea na kuanza kupaza sauti, “Bwana, Mwana wa Daudi, tafadhali nisaidie! Binti yangu ana pepo ndani yake, na anateseka sana.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, mama mmoja Mkaanani wa nchi hiyo alimjia, akapaaza sauti: “Mheshimiwa, Mwana wa Daudi, nionee huruma! Binti yangu anasumbuliwa na pepo.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, mama mmoja Mkanaani wa nchi hiyo alimjia, akapaza sauti: “Bwana, Mwana wa Daudi, nionee huruma! Binti yangu anasumbuliwa na pepo.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwanamke mmoja Mkanaani aliyeishi jirani na sehemu hizo akaja kwake, akilia, akasema, “Nihurumie, Ee Bwana, Mwana wa Daudi, binti yangu amepagawa na pepo mchafu na anateseka sana.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwanamke mmoja Mkanaani aliyeishi sehemu jirani na hizo akaja kwake akilia, akasema, “Nihurumie, Ee Bwana, Mwana wa Daudi! Binti yangu amepagawa na pepo mchafu, na anateseka sana.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na tazama, mwanamke Mkanaani wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, mama mmoja Mkanaani wa nchi hiyo alimjia, akapaza sauti: “Bwana, Mwana wa Daudi, nionee huruma! Binti yangu anasumbuliwa na pepo.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mara mwanamke wa Kikanaani aliyekaa mipakani huko akatokea, akapaza sauti akisema: Nihurumie, Bwana, mwana wa Dawidi! Binti yangu anapagawa vibaya na pepo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwanamuke mumoja Mukanana aliyeishi katika pande zile akamufikia, akilalamika, akisema: “Ee Bwana, mwana wa Daudi, unihurumie! Binti yangu anateswa sana na pepo.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na mwanamke Mkauanaya wa mipaka ile akatokea, akampaazia sauti, akinena, Unirehemu. Bwana, Mwana wa Daud; binti yangu amepagawa sana na pepo.