Matthew 15:27 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyo mama akajibu, “Ni kweli, Bwana; lakini hata mbwa hula makombo yanayoanguka kutoka meza ya bwana wao.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yule mwanamke akajibu, “Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yanayoanguka kutoka kwa meza za bwana zao.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mwanamke akasema, “Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula vipande vya chakula vinavyoanguka kutoka kwenye meza za mabwana zao.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Huyo mama akajibu, “Ni kweli, Mheshimiwa; lakini hata mbwa hula makombo yanayoanguka kutoka meza ya bwana wao.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huyo mama akajibu, “Ni kweli, Bwana; lakini hata mbwa hula makombo yanayoanguka kutoka meza ya bwana wao.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule mwanamke akajibu, “Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yanayoanguka kutoka kwenye meza za bwana zao.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yule mwanamke akajibu, “Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yanayoanguka kutoka kwenye meza za bwana zao.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huyo mama akajibu, “Ni kweli, Bwana; lakini hata mbwa hula makombo yanayoanguka kutoka meza ya bwana wao.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwanamke akasema: Ndio Bwana, lakini nao vijibwa hula makombo yanayoanguka mezani pa bwana zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule mwanamuke akasema: “Ndiyo, Bwana, unasema ukweli, lakini hata imbwa wanazoea kula makombo yanayoanguka chini ya meza ya wabwana wao.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akasema, Ndio, Bwana, illakini hatta mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao.