Matthew 15:3 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akawajibu, “Kwa nini nanyi hamjali sheria ya Mungu ila mnapendelea mapokeo yenu wenyewe?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akawajibu, “Mbona ninyi mnavunja amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akajibu, akawaambia, Mbona ninyi nanyi huihalifu amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akajibu, “Na kwa nini mnakataa kutii amri ya Mungu ili muweze kuzifuata desturi zenu?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akawajibu, “Kwa nini nanyi mnapendelea mapokeo yenu wenyewe na hamuijali Sheria ya Mungu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akawajibu, “Kwa nini nanyi hamjali sheria ya Mungu ila mnapendelea mapokeo yenu wenyewe?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akawajibu, “Mbona ninyi mnavunja amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akawajibu, “Mbona ninyi mnavunja amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akajibu, akawaambia, Mbona ninyi nanyi huivunja amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akawajibu, “Kwa nini nanyi hamjali sheria ya Mungu ila mnapendelea mapokeo yenu wenyewe?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, alipowajibu akisema: Nanyi sababu gani hamlifuati agizo lake Mungu kwa ajili ya mazoezo ya wakale wenu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akajibu, akawaambia, Mbona ninyi nanyi huihalifu amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akawajibu: “Na ninyi, kwa sababu gani munavunja amri ya Mungu kwa kufuata desturi zenu?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akajibu, akawaambia, Mbona na ninyi huikhalifu amri ya Mungu kwa mapokeo yenu?